Course Coordinator
JF-Expert Member
- Jul 27, 2019
- 1,683
- 3,070
Serikali ya awamu ya Sita iliachana na mfumo wa kujaza OPRASS kwenye makaratasi (nakala ngumu) badala yake ikatambulisha PEPMIS kupitia mfumo Employee Self Service kwa kifupi ESS.
Ikiwa na maana kwamba taarifa muhimu na za Msingi kuhusu Mtumishi zitakua kwenye mfumo huu.
Ikiwemo
Ikumbukwe mfumo huu ni Mpya na Elimu haijafikia watumishi hasa waliopo vituoni nikimaanisha kwenye Kata na Vijiji na wengi wao ni wale wazee wengine hata matumizi ya smartphone ni shida, mfano Watendaji wa Vijiji wale wa darasa la 7 , hata baadhi ya walimu hawajajua mfumo huu unavyofanya kazi.
Pamoja na changamoto lukuki kuhusu mfumo huu Serikali bado inachukua jukumu la kufungia mshahara wa Mtumishi wake aliyefanya kazi ofisini kwa siku 28 kisa TU hakujaza Sub Activity au Task na Sub Task kwenye mfumo kama kigezo cha upimaji , wakati kazini amehudhuria na amefanya kazi saa kiutumishi na muda mwingine amefanya kwa kupitiliza
Baadhi ya watumishi wanaangukia kwenye changamoto hii kutokana na Wakuu wao wa taasisi, mfano ikiwa Mkuu wa Idara/ Kitengo hakuwahi kukupa Role ama kwa kujisahau au kutokujua jinsi mfumo unavyofanya kazi maana yake mwezi husika hujafanya kazi kwa mwezi husika. Ikiwa hujaingia kwenye mfumo na huja submit sub task kwa Mkuu wako wa kazi unahesabika kuwa hujafanya kazi yoyote.
Pamoja kuwa Serikali ina nia nzuri kuleta huu mfumo isiwe kigezo cha kunyima watumishi mshahara kisa TU hawajapewa role na kujaza majukumu yao au kufanya tathimini kupitia mfumo huu.
Huu ni unyang'anyi usiotumia Silaha.
Baadhi ya Watumishi hao hao wamepanga wengine wanadaiwa kodi za nyumba.
Baadhi Watumishi hao wamefunga Kwaresima na Ramadhani wanahitaji kununua au kuwanunulia wazazi na ndugu zao chakula kwa ajili ya futari. Baadhi ya Watumishi maisha yao ni magumu hakuna mfano wanategemea huo mshahara kununua mahitaji muhimu Baadhi ya Watumishi wamekopa marejesho yanawasuburi.
Hii inaweza kuleta changamoto kwa baadhi ya Watumishi kuanza kuiba hasa kwa wakusanyaji wa mapato ya Serikali ikiwa ni kufidia mshahara wake aliozuiliwa na Serikali hivo kukosesha Serikali mapato.
Rai yangu
Serikali lipeni watumishi mshahara wa mwezi Machi, watumishi wengi watakaoumia sana sana ni wenye Mishahara ya chini.

- Kujaza majukumu na utekelezaji wa majukumu yao.
- Kupata salary slip kupitia mfumo huu
- Uhamisho na kupata mkopo kupitia mabenki husika.