SoC01 Serikali itumie wafungwa kama chanzo cha mapato. Iondoe Kodi inayokata kwenye Miamala ya Simu

Stories of Change - 2021 Competition

Livingson1

Member
Jul 13, 2021
30
26
Wafungwa ni watu wanaotumikia vifungo mbali mbali katika magereza zilizopo nchini Tanzania kote.

Wafungwa hawa wana ujuzi tofauti tofauti kwa kusomea ama kwa kujifunza mtaani, wengine ni engineers, nurses, wahasibu, doctors, mafundi kama fundi bomba, fundi nyumba, fundi kupaua, na wengine wana ujuzi wa kufanya kazi kwenye viwanda tofauti. Serikali inaweza kuwafungulia karakana na wakazalisha bidhaa serikali ikaziuza na kupata kipato.

Pia serikali inaweza ikashika tenda mahali mfano ujenzi wa nyumba, daraja, kiwanda na wafungwa wakaifanya hiyo kazi kwa ujuzi wao serikali ikapata kipato cha ziada

Lakini pia kuna wale wasio na ujuzi serikali inaweza kuwatumia katika uzalishaji kwenye mashamba ya serikali, kufanya kazi kwenye mashamba ama ranch za watu binafsi na serikali kupata kipato.

Serikali inaweza kuwatumia pia watu hawa kutoa elimu za mambo mbali mbali wanayojua hususani kwenye uzalishaji, ujasiriamali, n.k wananchi wakipata elimu hiyo watajiajiri na kuajiri watu wengine hapo serikali itapata kipato kwa malipo ya kodi za ujasiriamali
 
Back
Top Bottom