Zanzibar: Watu Watano wafariki, 12 wamelazwa baada ya kula Samaki aina ya Kasa

G-Mdadisi

Senior Member
Feb 15, 2018
157
99
Watu wawili wamefariki na wengine 11 kujeruhiwa Kisiwani Pemba baada ya kula samaki anaesemekana kuwa na sumu Katika Shehia ya Msuka Mgharibi Kijiji cha Taponi, Mkuu wa Wilaya anaeleza kila kitu

====

UPDATES: 28 NOV 2021

====

Tarehe 25 Novemba 2021 huko Pemba, Watu 25 wa familia tano walikula samaki aina ya Kasa ambaye kasababisha Vifo na Majeruhi.

Kamanda wa Polisi Kaskazini Pemba, ACP Juma Khamis ameiambia JamiiForums kwamba Watu Watano Wamefariki baada ya kula samaki aina ya Kasa. Kati ya Waliokufa ni Watoto wanne wa kuanzia Mwaka mmoja hadi 11 na Mtu mzima mmoja wa miaka 70 mwanamke.

ACP Juma kasema Watu 12 bado Wamelazwa na Watatu kati yao hali zao sio nzuri.

Kamanda amesema Serikali ya Zanzibar ilishapiga Marufuku ulaji wa Samaki aina ya Kasa na Bunju, kutokana na kuwa na Sumu, lakini bado watu wanawavua na kuwatoa baadhi ya viungo vyenye sumu kisha wanakula. Katoa wito watu kuepuka ulaji wa samaki aina ya Kasa na Bunju.
 
Mzazi wa waliofariki aelezea jinsi walivyopatikana samaki hao walioua.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa daktari dhamana wa hospitali ya Wilaya Micheweni, mtu mmoja mwingine amefariki usiku wa leo na kufanya idadi ya waliofariki kufikia watatu.

Naombeni maana ya neno kujeruhiwa
Nahis limetumika ndivyo sivyo hapo juu

Yan ule kitu upate jeraha??🤔
One sigala nipo hapa , neno jeruhi linaweza kutumika kiuhalisia au kihisia likawa na muktadha ule ule au unaoshahabiana naule kwa mfano mtu akisema nina jeraha la moyo hapo atakua ameongea kihisia lakini mtu akisema ana jeraha la mkono hapo pia unapata picha tofauti kwahiyo hapo aliongea kihisia zaidi
 
Out of question
 
Kuna tofauti kubwa kati ya kobe na kasa, Mi nimeshakuka nyama ya kasa ni tamu balaa. Halafu kuna kitu kimoja watu wanatakiwa waelewe, Kasa kama kasa hana sumu ila kuna wazungu wanawakata wanawadunga sindano za sumu then wanawaachi, sasa hao ndo wanakua na sumu. Nyama ya Kasa na ng'ombe haina tofauti.
Watu wanakula KOBE? Aiseee sawa.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya kobe na kasa, Mi nimeshakuka nyama ya kasa ni tamu balaa. Halafu kuna kitu kimoja watu wanatakiwa waelewe, Kasa kama kasa hana sumu ila kuna wazungu wanawakata wanawadunga sindano za sumu then wanawaachi, sasa hao ndo wanakua na sumu. Nyama ya Kasa na ng'ombe haina tofauti.
Ahaaa kumbe!maana kikawaida ukimatwa na kasa ni kosa kisheria na wapemba walikatazwa mda mrefu kutokula kasa.
 
Kuna tofauti kubwa kati ya kobe na kasa, Mi nimeshakuka nyama ya kasa ni tamu balaa. Halafu kuna kitu kimoja watu wanatakiwa waelewe, Kasa kama kasa hana sumu ila kuna wazungu wanawakata wanawadunga sindano za sumu then wanawaachi, sasa hao ndo wanakua na sumu. Nyama ya Kasa na ng'ombe haina tofauti.
Kwanini wanaweka sumu kwenye kitoweo hao mabeberu?
 
Back
Top Bottom