Benki kuu ya Tanzania(BOT) ni kweli mnalipa pesa za nauli kwa ubaguzi? Walimu wa Halmashauri ya Tunduru hatujalipwa tokea mwaka jana

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,173
6,156
Benki kuu ya Tanzania ni taasisi kubwa na yenye heshima kubwa. Kuna jambo silielewi, sisi tuna madai yetu ya pesa za likizo za mwezi wa 12 mwaka jana. Hatujalipwa mpaka leo. Tukifuatilia kwa uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru tunaambiwa maombi yenu tulishayapeleka BOT. Kwanza nataka kujua ni kweli kwamba BOT ndio walipaji? Km ndivyo kwanini baadhi walipwe na wengine tusilipwe mpaka leo? Maana ya hela ya likizo ni nini kwa mtindo huu? Maombi tuliyawasilisha

mwezi wa 11 mwanzoni ili hiyo hela itusaidie kwenda likizo mwezi wa 12 badala yake hamjalipa mpaka leo. Kwanini mnatunyanyasa watanzania ndani ya nchi yetu? BOT ndiyo wenye hela ya nchi hii kwanini wasitulipe?

BOT tunajua mna mishahara na marupurupu mikubwa sana mnayolipwa kwa kodi zetu, hivi vihela vyetu viduchu msitulipe kwanini? Mjue Mungu anawaona na hakuna aliyekufa na hela. Sisi walimu inajulikana mishahara yetu ni midogo sana na hatuna na posho yoyote kwanini hivi? Tulitakiwa tuende likizo mwaka jana mlitegemea tungeenda na nini, tumeshindwa kwenda kwa maana mmetupora haki zetu za kwenda likizo.

Mheshimwa rais kwanini raia wako tunyanyaswe ndani ya nchi yetu? Kisa ni walimu? Tunaambiwa nchi imekusanya trilioni 3 mwezi wa 12 sasa kwanini hamkutulipa? Na bado mpaka sahivi hamtaki kulipa. Hii imetuumiza sana. Mtu pekee wa kutusaidia ni wewe mh. Rais mama yetu Dr. Samia Suluhu Hassan
 
Sio kwamba pesa za nauli zinatokana na mapato ya ndani Halmashauri ? mnifundishe kitu hapa
 
Back
Top Bottom