BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Ni siku chache tu zimepita tangu itokee ajali ambayo haikuwa na madhara makubwa kati ya basi la mwendokasi na defender ya Polisi.
Picha za tukio hilo zilisambaa mitandaoni na ilivyoonesha wazi kabisa kuwa mwenye kos ani yule aliyekuwa akiendesha ile gari ya Polisi kwa kuwa aliingilia njia ya mwendokasi.
Sijui nini kiliendelea, lakini huo ni mfano wa matukio mengi ambayo yanahusisha magari ya Serikali au taasisi za Usalama ambayo yakiwa barabarani ni kama vile yenyewe yana upekee wa kwake.
Licha ya Serikali kusema mara kadhaa huko nyuma kuhusu madereva wa taasisi hizo kujifanya wao ndio wanajua kila kitu na wao ndio wababe, ni kama hakuna cha maana kilichofanyika kuhusu kubadilisha hali hiyo.
Tukio la jana 14/09/2022 lililoondoa maisha ya watu kadhaa akiwemo Mkurugenzi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, wapumzike kwa amani ndugu zetu hao, imeripotiwa kuwa dereva wa gari la kiongozi huyo aligomea kusikiliza kile kilichosemwa na askari wa usalama barababarani.
Nimeona wanasema alikatazwa kuingia barabarani kwa kuwa muda huo ulikuwa ni maalum kwa magari makubwa, yeye akabisha kwa madai ana haraka na wanataka kuwahi.
Hivi Serikali imeshindwa kufanya maamuzi magumu kuhusu madereva wao kuwa na tabia ya kutoheshimu sheria za barabarani?
Rais Samia na viongozi wengine wote hili kweli limewashinda au ndio ile kesi ya nyani unampelekea…..
Kuna wakati nawaza au labda madereva wanapata jeuri kwa kuwa wanasapotiwa matendo yao na haohao viongozi wao wanaowabeba?