Serikali: Hatujalipa kuweka tangazo jengo la Burj Khalifa lililopo Dubai

Msemaji wa Serikali kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema haya..

Serikali HAIJALIPIA kuweka tangazo la Tanzania katika jengo refu kuliko yote Duniani liitwalo Burj Khalifa lililopo katika Jiji la Dubai.

Tangazo hilo limewekwa kwa lengo la kuitangaza Tanzania kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi yetu na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Utawala wa Dubai umeweka tangazo hilo kwa kutambua ziara ambayo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kaifanya Dubai na umeahidi kuendelea kuitangaza Tanzania kupitia jengo hilo maarufu.

Pia soma

===
GHARAMA zilizoelekezwa na mamlaka ya uendeshaji wa jengo refu zaidi duniani la Burj Khalifa lililoko Dubai hutoza kati ya US$ 67,000 ambazo kwa ubadilishaji fedha kwa haraka haraka inafiki TZS 150M kwa dakika 3 kuweka tangazo kwenye jengo lote hilo la Burj Khalifa.

=>Gharama kwa lisaa limoja ni jumla ya TZS 3BL,

=> Gharama kwa siku moja ni TZS42BL

=> Gharama kwa siku 30 ni TZS 2.2Trilioni,

=>Kwasababu ya mahusiano mazuri kati ya mamlaka za Tanzania na Dubai tumepewa kujitangaza bure Kabisa kwa siku 30,

Nani Kama Rais Samia Suluhu Hassan?


Hoja yangu ni nini hapa,

Kwanza, Huu ni ushahidi wa wazi kwamba sasa ni rasmi Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefunguka Kitaifa & Kimataifa,

Pili,Kupitia matangazo haya Tanzania inakwenda kupata idadi kubwa sana ya wawekezaji wa nje na watalii ambao pengine haijawahi kuwashuhudia tangu Uhuru wake,

Tatu,Rais Samia anakuwa ni Rais mwenye ushawishi zaidi kusini mwa jangwa la Sahara ndani ya muda huu mfupi ( rejelea ziara zake za Ufaransa na Ubelgiji )

Nne, Burj Khalifa ni taasisi yenye zaidi ya followers 10M kwenye akaunti zake za Tweeter, facebook,Telegram na Instagram na nimejaribu kupitia accounts hizi Tanzania ina-trend kwa kasi,
Haya Endelea kutudanganya
 
 
Back
Top Bottom