FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 36,069
- 40,732
Ikifika mwezi wa 7 , kuna ‘mbuzi’ wawili au watatu watatolewa kafara, hii ni kwa decoding binafsi ya mtiririko wa matukio takriban matano hadi kumi niliyoya -observe, na inanipelekea kuamini hivyo.
1.) Haya majibu yanayotolewa na serikali kupitia Gerson Msigwa , Kassim Majaliwa na Hamza Johari yanatolewa kwa ajili ya nani? Maana tumeambiwa hizi kelele hazibadilishi chochote, sasa ya nini kutujibu wapiga kelele?
2.) Ni lini iliwahi tokea hapa Tanganyika pakawa na such an intense persistence, consistence na insistance ya kupinga matendo ya serikali kwa muda wa mwezi mzima bila kupumua, we are breathing bandari, day in , day out , hadi lini tutakuwa ignored?!
3.)Rais akiongea kwa sasa sauti yake inatetemeka, anaogopa nini, anaongea as if anataka kulia kwanini? Tangu lini mkuu wa nchi akatoa kauli irresponsible na ya kimipasho kama ile dhidi ya hoja serious kama za kuuzwa kwa Tanganyika, kwamba anaweka pamba masikioni?! Siasa ni Taarab?!
4.)Hadi majumbani watoto wanatuuliza tuufafanue mkataba huu wa bandari, imagine, kwa aibu kali inabidi tuwaeleze kwamba tumeuzwa kwa waarabu na waZanzibari, na huo ndio ukweli, wala sio udini au ubaguzi, ni ukweli tu., narudia kuziweka hoja hapo chini.
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)
2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?
3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!
6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
==========================
Maharage yameanza kurukaruka, bado kidogo tu...
Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Hakuna kipengele kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari, na hakuna mkataba wowote ulioingiwa
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi atoa maneno mazito mjadala wa DP World Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, amejitosa kwenye mjadala wa uwekezaji wa kampuni ya Dubai ya DP World unaotarajiwa kufanywa kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa kusema kuwa kuna...
www.jamiiforums.com
======================
Bado kidogo tu..
Tulia Ackson: Vifungu tulivyopitia vitaipa Serikali nafasi ya kuingia kwenye Majadiliano yatakayopelekea makubaliano na baadae Mkataba
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson amesema wao kama wawakilishi wa Wananchi wamepitia Vifungu vyote kimoja baada ya kingine na wamejiridhisha havina shida yoyote kwa sababu vinaipa Serikali nafasi ya kuingia kwenye Majadiliano yatakayopelekea Makubaliano na baadae...
www.jamiiforums.com
======================
Masikio yanaanza kuzibuka
Waziri Mkuu: Tumesikia mijadala, hofu kuhusu makubaliano ya Bandari. Tumeanza kutoa elimu ya kuwapa faraja Watanzania
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amekiri kuwa ni kweli tangu Bunge la Tanzania liliporidhia azimio la Nchi ya Tanzania kuimarisha mahusiano yake Nchi ya Tanzania na Nchi ya Dubai hasa katika maeneo ya Kiuchumi na Kijamii, kumekuwa na mijadala mingi, maoni, ushauri na hofu za Uwekezaji nchini...
www.jamiiforums.com
==========================
Update: 24/07/2023
Sekretarieti ya Bunge: Kuna mapungufu katika Mkataba wa Bandari na DP World; ukomo wake uwekwe wazi
Kwa furaha kubwa kabisa napenda kuwataarifu wana JF kuwa kwa tukio litakalotokea leo tarehe 24/07/2023, mjadala wa Dp world ndio unafika mwisho, tujipongeze wote tulioshiriki. Ahsanteni sana. ========== Mdau mwingine pia aliandika: Tumelumbana weee, tumeelezana weee, Kuna wale vichwa maji...
www.jamiiforums.com
========================
18/08/2023
Tetesi: - Muda wowote kuanzia sasa Samia ataachana na DP World!
Be the first to know... muda wowote kuanzia sasa Rais Samia atauzima rasmi mjadala unaochukua sura mpya kila siku nao si mwingine bali ni DP World! Vyanzo vyangu toka ndani ya Chama na Serikali vinabainisha joto la mjadala linaelekea pabaya hivyo busara imetumika kufunika kombe mwanaharamu...
www.jamiiforums.com