benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Leo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ummy Mwalimu ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu inakwenda kuandika historia kwa kufuta suala la wanafunzi wanaoingia kama changuo la pili na la tatu (Second and Third Selection) kutokana na upungufu wa madarasa.
Waziri Ummy amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha hela za ujenzi wa madarasa zilizotolewa kwa kila Wilaya na Mkoa nchini zinatumika ipasavyo kuhakikisha ujenzi wa madarasa unakamilika ifikapo Disemba 15 mwaka huu.
Kwa hatua hiyo ina maana kwamba mwaka ujao wa masomo wanafunzi wote wa kidato cha kwanza wataanza masomo kwa pamoja jambo ambalo halijatokea nchini kwa kipindi kirefu.
Kama hili likitimia kwa wakati na ubora basi ni dhahiri neema itakuwa imeanza kurejea nchini. Baada ya hapa sasa nadhani jitihada zipelekwe kwenye kuinua hali ya maisha ya walimu na kuwapa vitendea kazi na makazi mazuri.