Serikali awamu ya sita inalipa mishahara mapema kabisa tarehe 22, imevunja rekodi ya Hayati Magufuli wa akilipa tarehe 25 mpaka 27. Hongera Rais Samia

Wastaafu wamelipwa? Niko msibani hapa kuna mstaafu anasema hana cha kuchangia Pension haijaingia hadi muda huu tarehe 25 na msiba ni wake
 
sasa mchape kazi kwa bidii na maarifa yenu yote, muache kupigana mjungu na fitina.

Rais Samia kadhamiria kurudisha tabasamu kwa watumishi wa umma, sasa kamwe hawataishi maisha ya kukopakopa na kudhallika kwenye maduka ya vyakula.

Pongezi pia kwa Waziri Jenista Mhagama kwa bidii anayo ifanya ya kuwaboreshea masilahi ya watumishi.
Bajeti ya mwaka 2022/23 inajambo kubwa kwa watumishi.

Mbunge wa Gairo aliwahi kusema
" ukitaka mzunguko wa fedha uongezeke basi waongezee mshahara watumishi wa umma kwani wao ndio walio tapakaa kila kona ya nchi na ndio wenye matumizi makubwa........"
kweli mkuu kwani bajeti inayoishia mishahara ya watumishi ni trilioni ngapi na bajeti ijayo propose budget ni shilingi ngapi tuanzie hapo tujue kuna nyongeza ya asilimia ngapi
 
Back
Top Bottom