Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Utawala wa Awamu ya sita ulianza rasmi tarehe 17 mwezi machi mwaka 2021, Rais Samia alichukua kiti cha Uongozi baada ya kifo cha JPM.
Katika miezi hii 9 na ushee Mama huyu alipochukua kiti cha Uongozi napenda kusema nimeridhika kwa namna ambayo analiongoza Taifa letu pendwa la Tanzania. Amepata mafanikio mengi pamoja na kuwepo kwa changamoto za hapa na pale.
Mafanikio
1. Kiuchumi
Baada ya mkwamo wa miaka kadhaa kutokana na magomvi baina ya Tanzania na majirani zake. Rais Samia alipoingia madarakani jambo la kwanza alilofanya lilikuwa ni kuboresha mahusiano baina ya Tanzania na majirani zake. Kuboreshwa kwa mahusiano haya kumeenda kusababisha Tanzania kuongoza Kwa kuuza bidhaa kwenye Mataifa ya Uganda na Kenya kwa Mara ya kwanza kwenye historia za mataifa haya. Ripoti za Benji kuu za Uganda na Kenya katika mwezi July na Agosti zilisema haya. Haya ni mafanikio
Katika kipindi cha miezi michache aliyokaa madarakani fedha ya Tanzania imepata nguvu zaidi dhidi ya Sarafu ya marekani jambo ambalo Kwa wabashiri wa masuala ya kiuchumi wanasema ni taa ya kijani kwake katika kuipa Tanzania Uchumi mkubwa na kuongoza kiuchumi katika kanda hii ya Afrika Mashariki na Kati katika siku zijazo!
Kwa upande wa hifadhi yetu ya fedha za kigeni chini ya Utawala wake ameomgeza zaidi hifadhi yetu na kutufanya tuongoze kwa Mataifa ya Afrika Mashariki kwa sasa!
2. Kiutalii
Kutokana na kufuata taratibu mbalimbali za kuepukana na corona Tanzania ilishuhudia kupokea watalii wengi zaidi katika kipindi hiki kuliko ilivyokuwa mwaka jana kipindi hiki. Taarifa zinasema mapato ya italii kwa kipindi hiki tu yamepanda kwa zaidi ya Trilioni 1 baada ya Tanzania kupokea watalii laki Saba na ushee ikiipiku kenya katika kipindi cha mwisho cha mwaka huu!
3. Elimu!
Kwenye Elimu katika kipindi hiki kifupi cha Awamu ya sita , Taifa limeshuhudia ujengwaji wa madarasa Bora kabisa Kwa ajiri ya kusomeshea watoto wetu! Ilionekana Kama masikhara ila kwenye kipindi kifupi sana, Taifa letu limeshihudia madarasa mazuri yenye mazingira mazuri sana yakijengwa Kwa ajiri ya watoto wetu. Ingawa watu wanasema pesa hizi ni za mkopo ila ukweli lazima usemwe! Haya ni matumizi safi na Bora zaidi katika kuboresha mazingira ya elimu yetu . Amefanya vizuri sana kwenye hili
4. Miundombinu!
Katika miundombinu amerudi kufanya vizuri sana! Hakuna mradi hata mmoja aliorithi kutoka kwa mtangulizi wake ambao umesimama. Amekamilisha ujenzi wa daraja la Tanzanite, Ujenzi wa Barabara ya Morroco - Mwenye, ujenzi wa Barabara za mji wa Serikali Mtumba ambazo Mtangulizi wake alifariki akiziacha sehemu kubwa zikiwa za vumbi. Ameendeleza ujenzi wa Awamu wa pili wa mji wa serikali na sasa ukiwa Mtumba kila sehemu utakuta ni mabati ujenzi ukiwa unaendelea.
Kwenye Bwawa la Nyerere nako hakujasimama, mafundi wako site wanaendelea na kazi, SGR nako hakujapoa kipande cha Dar - Moro amekikamilisha na sasa kinatarajiwa kufunguliwa muda si mrefu. Amesaini Mikataba ya ujenzi wa vipande vya Dodoma- Tabora na ameanzisha ujenzi wa Mwanza - Isaka.
5. Hospitali
Kama ilivyo kwenye elimu hapa napo Mama Samia hajalala. Ameendeleza na kuanzisha ujenzi wa vituo vya afya, zahanati pamoja na hospitali nyingi sana. Amenunua vifaa na magari mengi kwa ajiri ya hospitali mbalimbali. Huku amefanya kwa kutumia fedha za tozo pamoja na fedha za mkopo wa covid. Amefanya vizuri na hongera kwake
6. Miradi mipya
Pamoja na kufanya na kuendeleza vizuri bila kupoa. Samia ameanzisha miradi mipya. Mradi wa LNG ambao ameanzisha mazungumzo pamoja na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ambao pia ameanzisha mazungumzo. Kwa wachumi miradi hii miwili ndo inatarajiwa kuwa breakthrough ya Tanzania kiuchumi. Anafanya vizuri na ana malengo mazuri!
7. Ubunifu mpya kwenye Utalii
Baada ya malalamiko ya miaka mingi juu ya Taifa la Tanzania na serikali zake kutotumia vizuri fursa za kiutalii ambacho ni moja ya vyanzo vizuri na vikubwa vya mapato kwa Mataifa mengi Duniani, Samia ametumia ubunifu wake kwa kufanya kipindi cha The Royal Tour. Kipindi hiki kinatarajiwa kuiweka vizuri zaidi Tanzania katika ramani ya utalii duniani na kikishaznduliwa kinatarajiwa kuvutia watalii zaidi ya Mil 5 katika nchi hii kwenye miaka ya hivi Karibuni. Kwa hili pia amefanya vizuri sana
8. Ajira
Baada ya kukwama kwa ajira kwa karibu miaka 5 , serikali ya Awamu ya sita kwa miezi hii 9 tu wametoa ajira zisizopungua elfu 15 kwa serikalini tu. Ajira hizi zimetolewa jwtz, magereza, polisi, uhamiaji, zimamoto, pccb na Tra. Pia ametoa ajira za walimu na madaktari. Kwa hili hongera Sana Rais Samia
Changamoto
1. Hujuma kutoka kwa watu wasiomkubali
Hapa amekuwa akipata hujuma kutoka kwa kundi linalojulikana Kama Sukuma Gang ambao hawa hawakutaka awe Rais. Wamekuwa wakimuhujumu kupitia sekta mbalimbali Kama nishati kama kukata umeme hovyo ili kumchonganisha na wananchi wake. Kwenye umeme kundi hili kutokana na kuwa na uhusiano na watu fulani wamekuwa wakuhujumu Tanesko na kusababisha kukatika kwa umeme katika maeneo kadhaa hapa Tanzania. Inasemwa hata katika mikoa ya Rukwa na Katavi ambako umeme ni wa kununua kutoka Zambia nako umeme umekuwa Uko katika kutokana na hujuma tu za kundi hili.
Ni vizuri waziri wake Makamba na watendaji wapya wa Tanesco wakachukulia kuwa hii ni vita na sio vile wanavyoona na wakachukua hatua kali ili kudhibiti hili. Ni vizuri na vyombo vya ulinzi na Usalama vikahusika katika kushughulikia hizi hujuma
2. Kupanda kwa bei za bidhaa
Ingawa hii inaweza kuwa imechangiwa na janga la Corona Ila kwa sehemu fulani Kuna kauzembe kwa watendaji wake katika kuzuia uholela kwenye hili hasa katika Bei za mafuta ya kula, sukari, sabuni na vifaa vya ujenzi.
Hapa akiwabana vizuri Mawaziri wake wa viwanda na biashara anaweza pata suluhisho kwenye hili maana wanaoneka wamerelax sana katika kuzuia hili
Mwisho napenda kuipongeza Awamu ya sita. Si kazi ndogo kuongoza Tanzania lakini mmeonesha mnaweza. Sijagusia kwenye ulinzi na Usalama ambako nako mbao Beka aso dar mko vizuri Ila kiukweli keep it up. So far mko vizuri