Hiyo Planet Earth ni documentary, mimi sio mpenzi wa documentary TV Series, ndio maana sijawahi kuiangalia mpaka leo. Ila top ten ya IMDB ukiondoa documentaries, nimeshazitazama, na kwa mtazamo wangu hawajakosea katika "kuzirank". Kuna wakati huwa nafikiri sisi "Wabongo" huwa hatujui TV Series nzuri, hiyo nahisi inachangiwa na level of INTELLIGENCE, Wabongo tunapenda TV series ambazo zina matukio mepesi kuyachakata, ndio maana wabongo wengi ni wapenzi wa action movies/series, ndio maana ni rahisi kukuta mtu anakuambia Money Heist ni kali kuliko The Wire au Strike Back ni kali kuliko Breaking Bad, wakati ukweli ni kuwa The Wire na BB ni kati ya TV series kali kabisa kuwahi kutengenezwa hapa duniani. TV series karibia zote ambazo zinachukuliwa kama kali kuwahi kutengenezwa, sio "popular" mtaani au humu jukwaani, tukiondoa mapenzi binafsi, sababu ni hiyo niliyokuambia hapo juu (Level of intelligence).