Series (Special thread)

niliangalia mpaka pale anapomuua baba yake yule binti anayependa kufanya naye mission
Daaaah! Basi pale ilikua mwanzo na hujui kua yule binti ambaye anajulikana kama Elizabeth Keen anayependa kufanya nae mission ana mume wake ambaye unamuona wa kawaida lkni yule ni hitman na katumwa pale kwa lengo maalum
 
😳😳😳 So unataka kusema ni kali kuliko money heist maana ukitaja series za Netflix ukifikiri haraka haraka money heist ndo inakuja kwenye vichwa vya watu?
Itafute Dark Broh. Ukishamaliza kuicheki, niambie umeona nini, lakini nina uhakika utaipenda tu, coz ninavyofuatilia huu uzi nimeone series nyingi ninazozikubali na wewe unazikubali pia. Ila naweza kusema tu, ingawa naifuatilia vyema Money Heist lakini ipo wazi kuwa Money Heist ni Netflix overrated series. Kwangu mimi Netflix hawajawahi tengeneza series kali kama hii kitu ya kuitwa Dark. Lakini huu ni mtazamo wangu binafsi.
 
Chief, mimi hiyo kitu ya Blacklist sichoki kuifuatilia kwasababu ya shauku ya kutaka kujua huyu Red ni nani haswa! Kuna wakati nilihisi Reddington ni Katarina Rostova, lakini nilivyoanza kuangalia season ya 7 nakuta Katarina yupo hai na anaishi Ufaransa basi nikaishiwa pozi kabisa. Ila nitaendelea kuifuatilia mpaka mwisho ili nione kama huyu mtu atakuja kujulikana ni nani, na sababu za yeye kuamua kuwa Reddington ni zipi, pia alikuwa na mahusiano gani na Reddington halisi. Kuna wakati pia najisemea kichwani, usikute huyu Reddington ni Reddington halisi ila Katarina Rostova ndiyo imposter, ila mfululizo wa matukio unaikataa hii nadharia yangu.
So far nipo nipo Season ya 7, episode ya kwanza, ngoja niendelee nayo.
 
Nimeshashusha season zote 3 Ila nasubiri nimalize The walking dead season 10
 
Hahahahaha mkuu hayo maswali unaojiuliza wew ndo najiuliza mim na nimemaliza season ya 7 nimepata swali lingine Ila ngoja nikuache uendelee uone battle kati ya Reddington na Katarina humo wanavyoshindana kwenye kufikiri, kufanya missions na story Reddington aliyoeleza kwenye seasons za nyuma kuhusu Katarina sio kweli mzee hadi nimebaki na swali tena
 
Episode ambayo itakuja kuweka wazi ukweli kuhusu Reddington itawaacha watu wengi midomo wazi. Upendo wa Reddington kwa Elizabeth sio upendo wa kawaida, hii inanifanya nishindwe kuamini kuwa Red ni mtu baki tu. Reddington yupo tayari kuua mtu yeyote ambaye anaifahamu siri yake isipokuwa Liz na Dom (Babu yake Liz), kwanini? Kuna siri kubwa sana hapa mkongwe.
Ngoja nimalize mzigo wa Dark kwanza, then nitaendelea na hiki kigongo cha The Blacklist.
 
thanks
nitaitafuta tena hiyo project
 
Ndo nakomaa nayo hapa naona imeanza kua moto
 
Sio Elizabeth na Dom tu hata yule jamaa Frank bloom ambaye alikua mtu anaeaminiwa na Katarina Rostova nae anaogopa kutoa Siri kitu ambacho kilinishangaza pia. Sema haina noma mzee ukweli utafichuka tu iyo s08
 
Quantico umeshaicheki mkongwe? Kama umeshaicheki nahitaji kujua unairate aje, inastahili kuchukua muda wangu kuitazama, au ni utopolo tu?
Quantico Inaanza na story nzuri kuanziaa s01 na nikaipenda s02 kwasababu kwa 90% wametumia lugha yetu ya kiswahili Ila sikuendelea nayo coz walikuja kuharibu kwa kuleta story ambayo hainivutii kwa upande wangu kama ilivyo Designated survivor ambayo s01 ilikua kali kinoma Ila s02 ilikua chenga kwa kuleta usiasa wa kimarekani mwingi
 
Must see series top imdb
When they see us
zerozerozero
The spy
Fauda
Gangs of London
Ntatoa link ya telegram PM kuzipata izo series HD quality kwa walio interested
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…