Series (Special thread)

The Punisher nimeikubali..marvel nawakubali sana.
 
Nimeangalia season nyingi ila hizi za ki intelligence ndo kiboko..
>>>Prison Break
>>>24 Hours, hii imebidi nianze mwanzo ndo nipo Season 4
Huyu Chloe O'Brian nampenda sana Hasa akiwa kanuna.

>>>3Days hii nayo kiboko Han Tae Kyong alinikosha sana alivyokua anamlinda Raisi..
 
Vikings season 5 returns Tomorrow

Kati Ya Series Ambayo Kila Nikiangalia Huwa Natabasamu Na Sijajua Kwa Nini,Ilifikia Hatua Mpaka Niliimisi, Nilivyosikia Inarejea Tena Nikajikuta Natoa Tabasamu La Nguvu Yaaani, Kati Ya Series Ninazo Zikubari Sana Sana..
 

Producer .. Anasimamia na kuongoza uzalishaji wa fulamu. Ndio tuseme CEO wa production.. Anajua nani atafaa kuwa Director.. Nani atatafuta waigizaji fedha zitatoka wapi..mauzo na matangazo yatafanyikaje nk

Mara nyingi wanakuwa na Ass. Producers katika miradi inayokuwa mikubwa sana.

Story+scripting hii inafanywa na kundi la watu.. Wanaoangalia mambo mengi madogo madogo ila muhimu katika filamu.. Vitu kama dialogue, monologue, portrayal of characters (Tabia zao) no hapa kunakuwa na director, mtunzi wa story au hadithi(kwa sehemu ambayo kitabu kinatumika). Kwa sehemu zingine watunzi sio lazima wawepo ila jopo la wataalamu wanaweza kuja na script has a kwa movie za genre ya Documentary.

Director:- huyu ndio mpishi.. Huyu anajua lengo kuu lafilamu na anakuwa na uwezo wa kuiamuru kwa vipande vipande iletwe kupitia camera movements, mwanga, uigizaji na maelezo. Hutu anaijua filamu ikiwa kichwani mwake na anajitahidi kuzielekeza element nyingine za uzalishaji ili zifikie lengo alilonalo kichwani.
 
Ukweli kabisa.. Waongozaji, waandishi ..na cinematographers wakibadilika..hasa waongozaji kunauwezekano filamu zikakua. Itabidi nijitose some day..tusijeonekana tunaongea tu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…