Series (Special thread)

Bora hiyo kwakweli 😁😁

Superheroes kwakweli hapana. Japo zipo chache kama wonder woman ya kwanza, superman, Deadpool, na daredevil naweza kuziangalia (sijajua kama nimepatia hiyo category ya superhero)
😅 Ndio zenyewe, kumbe unaweza kuangalia jaribu na nyingine utazipenda, we angalia story usianze kuwaza mtu anawezaje kupaa kweli 😁
 
Rafiki yangu mkubwa, ambae kwa sasa naweza sema urafiki umepungua sana (maybe sababu ya step ya maisha niliyomzidi), yeye ni idealist sana.. alikua akiniambia mara kwa mara niitazame hii movie ina funzo kubwa sana ila nilikua nikiipotezea..

Ilikua kila nikimuuliza aniambie what is it about, and if possible anipe funzo lililopo alikua hataki kabisa aki insist niiangalie ila sikupata hiyo nafasi.

Sasa baada ya kusoma hii comment yako naona kuna sababu ya kuitafuta, maana jamaa alikua ana insights sana na miaka kadhaa nyuma nilikua nina ujinga ujinga sana.. kuna kitu alitaka nipate kutoka humo. Guess I'll find out..

Thanks champ!
 
ni kwanini marafiki wengi wakizidiana hatua flani katika maisha, otomatik urafiki unakufa ama unapungua kabisa..!?
shida inaanza kwa ‘mfanikiwa’..!? ama shida huwa zaidi kwa ‘mfanikiwi’..!??
 
ni kwanini marafiki wengi wakizidiana hatua flani katika maisha, otomatik urafiki unakufa ama unapungua kabisa..!?
shida inaanza kwa ‘mfanikiwa’..!? ama shida huwa zaidi kwa ‘mfanikiwi’..!??
Story of my life, nimempoteza my childhood and a bestfriend kimasikhara masikhara tu baada ya kumtangulia kufika pale ambapo wote tulikua tunaomba kufika, nilidhan angekua proud matokeo yake akashindwa kuificha chuki yake kali dhidi yangu, imagine nimemfahamu my whole life.
 
Pole dear,
sijui ni kwanini lazima tupitishwe huko, mimi huyo wangu alinipiga matukio balaa, kwanza mpaka kujua anayonifanyia alishafanya damage kubwa sana kwenye maisha yangu..!
 
ni kwanini marafiki wengi wakizidiana hatua flani katika maisha, otomatik urafiki unakufa ama unapungua kabisa..!?
shida inaanza kwa ‘mfanikiwa’..!? ama shida huwa zaidi kwa ‘mfanikiwi’..!??
Shida inaweza kuwa chuki kama alivyosema Dr. Mariposa ama muda mwingine inakuwa aibu, kuna watu wakiwa na shida ni bora akope kwa mtu asiye mfahamu vizuri kuliko kwa ndugu yake au rafiki yake,
 
Kuna SPA ipo mwz inaitwa Mariposa beauty parlor au ni yako🥹
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…