Series (Special thread)

Bianca hajafariki
Yule kashadedi aisee. Kwa ule muda aliolala pale chini, damu inatoka mdomoni, na Jackal kamuacha tu vile...keshaenda mbinguni yule.

Labda kama waweze kutuaminisha kuwa Jackal alimuokoa akamficha mahali na kumpa uangalizi. Hii haiwezekani maana jamaa nae alikuwa busy kumfuatilia make wake aliyetoroka nyumbani...

Wanaweza kuispin hii story iwe kwamba Bianca na Jackal wawe rogue antiheroes wakishirikiana kupambana na wale waovu wa ukweli kwenye system kama yule Lannister na yule Minister, huku Osita akiwapa support kwa siri ndani ya Section 303...
 
View attachment 3175481

Hivi huyu mzee haogopi kumfanyia udhurumati The Jackal mtu mbayaπŸ˜‡

Risasi moja tu ya jicho kutoka kwa mwamba Jackal inamhusu.

Season 2 jamaa atakuwa anatoroka nchi na private jet baada ya msako mzito kutoka kwa Zina upande mmoja na MI6 agents kadhaa kwenye ma Range meusi waliokuwa wakimfukuza barabarani na yeye kuingia kwenye parking building na kubadilisha magari na kuwapoteza.

Atafanikiwa kuingia kwenye ka airstrip cha don mmoja mwenye winery nje ya mji kwenye kashamba flani ka mizabibu. Atatoka kwenye hangar vizuri tu na ki Gulfstream G8 chake na kuclear runway vizuri tu, ila ndege ikiwa hewani na ka stewardess kakiwa kana mmiminia champagne, ghafla mlango wa rubani unafunguliwa na rubani anatoka. Rubani ni nani? Jackal mwenyewe.

Wanaongea mawili matatu halafu Jackal anampiga ile "F@#k you" kama ya kale katapeli kengine ja kijerumani na kumpiga moja ya jicho.
 
Kale ka jerumani kalileta makuzi kale πŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Kale ka jerumani kalileta makuzi kale πŸ˜€πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ

πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ kabisa aisee. Halafu kanatoa sababu ya kijinga kabisa kwamba eti kalikasirika kwa sababu Jackal alikashoot. Yaani mtu kakutumia kama chambo na matokeo yake ni amekuweka katika nafasi nzuri kisiasa kuliko ulivyotarajia, halafu humlipi eti kisa umekasirika.

Mwanasiasa gani asiyeelewa kwamba 'the end justifies the means'?

Kale kasingeweza kuachwa salama kabisa.
 
Wenzetu sijui wanatengenezaje hizi series zao yaani wanakuteka akili unajikuta

Unampenda mtu au kumchukia Ile toka moyoni, baadae unajishaangaa unakumbuka kumbe nacheki muvi😁
Umakini na Uthubutu, series inatengenezwa miaka kadhaa ndio inaachiwa.

Sio hawa wenzetu kila weekend wanaingia site kutuleta episodes za wiki nzima inayokuja.
 
Yep, sio rahisi character wampe na Familia kabisa, (mume na mtoto) halafu wamuue kizembe vile, Pia bado Bianca kuna kitu anatakiwa kujifunza.
 
Tatizo mnaangalia series hamfatilii habari za huko Kwa platform nyingne.

Bianca alishakufa mana ule msemo wa tumuache aende Spain then sisi tutajua namna ya kudeal nae walijua tu tutamfahamisha mwamba na hatoweza kuwaacha salama this time.

Kwa habari njema season tu ishaanza kuandaliwa ila hawajaanza kushoot.

So tusubir mwaka ujao mwshon au 2026.
 
Kuna kameseji kakikuda bianca alimtumia afisa mwenzake. Sema afisa ni.mwoga kinoma alifuta palepale
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…