Serengeti: Tundu Lissu akumbuka shambulio dhidi yake, amtaka Rais mpya na IGP mpya kuwakamata Wahusika

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,288
219,523


Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi kwenye mkutano Mkubwa wa hadhara , Makamu Mwenyekiti wa Chadema , amesema kwamba , Tangu aliposhambuliwa kwa Risasi hakuna yeyote aliyekamatwa wala hakuna uchunguzi uliofanyika hadi sasa .

Amedai kwamba hapo awali , alidhani haukufanyika uchunguzi kwa vile aliyewatuma wauaji wakati huo alikuwa Rais , kwahiyo ingekuwa vigumu kujikamata na kwamba IGP wa wakati huo alikuwa Sirro , lakini sasa Rais ni Samia na IGP ni Wambura .

Tundu Lissu ameendelea kuhoji kwamba , Sasa kama viongozi wale wa zamani wamebadilika na wale wabaya wameondoka , hawa wema akiwemo tunayesema NANI KAMA MAMA , Mbona wahalifu hawa hawakamatwi ?

Ujumbe wake huu hapa

 
Kama anathibitisha aliewatuma wauaji kafa, watamkamata nani sasa? Yeye akitaka aseme aliyewatuma kafa, ila waliotumwa wapo ambao ni fulani na fulani. Wakishaitwa nao watasema kama walitumwa kweli au hapana.
 
Mtuhumiwa kafa Sasa hapo Kuna kesi gani? Maana ndio anawajua aliowatuma
 
Awataje wakamatwe
 
Hivi Rais Samia anaanzaje kuanza kuwakamata waliomshambulia Lissu mwaka 2017 kwa namna anavyomtukana majukwaani.

Hili jitu kweli lilishambuliwa na watu wa Magufuli lakini halina shukrani. Wachana nalo
 
Hivi Rais Samia anaanzaje kuanza kuwakamata waliomshambilia Lissu mwaka 2017 kwa namna anavyomtukana majukwaani.

Hili jitu kweli likishambuliwa na watu wa Magufuli lakini halina shukrani. Wachana nalo
Rais Samia ni mwanasiasa Lissu ni Mwanasiasa pia. Mashambulizi ya kisiasa ni jambo la kawaida.

Mbona mnataka kumdogosha Rais? Kwamba asisemwe? Akisemwa mnadai eti ni mwanamke.

Rais ni Mtu Mkubwa kwenye Nchi anapaswa kujibu hoja zinazoibuliwa upande wa pili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…