Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Baba Mchungaji. Asante sana kwa sala hii yenye nguvu na upako. Nimeguswa sana!

Hakuna zawadi ya thamani zaidi ya maombi na hakuna njia bora ya kumjali mtu zaidi ya kumuombea. Hebu yote uliyoyaomba juu ya maisha yangu na yakapate kibali mbele ya Mungu wetu Aliye mkuu. Mungu huyu mwema Amenivusha katika vita vikali vya kiroho na kimwili na naamini kuwa ana makusudi mema na maisha yangu. Na bahati nzuri najua ninachotakiwa kufanya na naamini kitatimia. Ndiyo maana niko hai!

Wewe ni mdogo wangu kiumri na nakuhesabu kama ndugu. Mungu Atupe uzima na naamini siku moja tutaonana na kusali pamoja. Barikiwa sana Mtumishi...

Maombi yametolewa na kama manukato na marhamu ya thamani sana yamepanda na kufika mbele ya kiti cha enzi; na yamepokelewa. Shetani ameshindwa na ushindi umeshapatikana tayari.

Tubaki katika rehema na kumbato lake nasi daima tutabakia salama kwa sababu Alishaahidi kuwa hatatuacha. Tutubu madhambi yetu. Tupendane. Tusameheane na tuonyeshe upendo na tumaini lake kuu kwa wengine...

Asante sana Baba Mchungaji
View attachment 2230138
Ni ndugu, kaka yangu, na wapendwa katika Kristo. Maisha yana history.. Kitu kizuri Mungu alituita kabla ya kuwekwa misingi ya dunia ( Mungu analinda kusudi lake ndani yetu kwa kuachia neema na rehema ) Mungu anaangalia mbele yetu na sio nyuma ( mapito yetu ) yeye Mungu nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.

Tuna wengi Apostle Paul history yake ilikuwa kama unavyojua Apostle Peter , Prophet Isaih.. kuna nyakati Mungu anaruhusu tupite mahala ilikuunda picha yake ndani yetu na kuelewa na kutufanya kuwa humble.. binafsi issue pekee ambayo nilikuwa na strugle nayo miaka na miaka na nilikuja jifunza badae kwanini nilikuwa nina strugle hapo .. ili nifanye niwe na hofu na Mungu na kumuogopa na kujua haikuwa kwa uwezo wangu kutoka pale bali Mungu ali ruhusu ili nijue kabisa kwamba yeye ndio mkombozi wangu, nilikuwa na Utakatifu na mtazamo wa utakatifu wa hali ya juu sana kiasi kwamba nikawa najiona kama Mungu, ndipo nilipo anza chezeshwa na zambi moja tuu hadi nilikoma ilifika kipindi nilikuwa nakataa tamaaa completely nilifanya kila nilichoweza waaapi funga waapi ombaaa waaapi .. kupitia haya mambo ana tutengeza 😀😀😀
 
Back
Top Bottom