Msukuma jamani.
Anyways niwatake radhi single men wote wa humu. Jamani tulianza kama utani kwamba wote humu mmeshaoa; coz sio kitu cha kweli. Personally nawafahamu vijana wengi tu huku ambao hawajaoa; so please ambao tumetishia "ndoano" zenu mtusamehe bure. Utani uliogeuka kuwa a serious talk along the way.
Kukumbushana ni muhimu kwa kweli hata kama hakuna under 10 humu. Yes kama nilivyosema kama umeoa/umeolewa au una mahusiano yako serious na umekutana na mtu na ukamtamani; mwambie tu ukweli ili ajue kusuka au kunyoa.
Kuna wanawake ambao wao naturally wanataka married men; so ukiwaambia ukweli wanakupokea kwa mikono miwili; they have nothing to lose. Au mwingine ajijue ni mchepuko akuchune kimahesabu au afanye makaretee ya kumpindua mkeo.
Kuna watu ambao wapo serious na wanahitaji mahusiano serious; hawana muda wa kupoteza. Huyu ukimdanganya kuwa hujaoa/olewa, akainvest kwako na kuachana na wote; afu baada ya miaka 2 ndiyo anakuja kushtukia kuwa umeoa/kuolewa aisee sio haki. Ni kumpotezea mtu muda na kumuharibia maisha yake. Imagine binti amebeba mimba ndiyo anagundua mwenzie ni mume wa mtu na katu hawezi kumuoa; anaishia kuwa singo mom na mtoto wa kufichwa juu.
Kuna binti December alikuja kulipiwa mahari; harusi ilikuwa soon after Easter. Vikao vimeshaanza kabisa; mara ghafla anapokea simu mtu anajitambulisha kama ni mke wa huyo mchumba wake. Akamtumia na copies za vyeti na picha za familia; kumbe mume alihamia kazi mkoa mwingine ndiyo kafika huko na kuwa MBA. Uchumba ikabidi uvunjwe; imagine how traumatized that lady is. Tusijitafutie laana zisizo na msingi
So tuwe tu wakweli; kuna kina Coca wao hawajali. Uwe tyuuu na ndinga siku mojamoja akanyage mafuta na kujisnap; muende hotels zenu n.k . Siku ukimuacha kwa raha zake anarudi zake kwenye daladala/mwendokasi kwa amani kabisa as anajua kuwa success isn't sexually transmitted. (coca nakutania mwanangu, usinichambe mama ako)