Heaven Sent
JF-Expert Member
- Sep 27, 2013
- 32,717
- 98,376
Msukuma jamani.Dunia hii mhh!
As long as wahusika wote ni watu wazima (18+) na wanadanganyana kwa hiari yao mpaka wanakutana na hatimaye kujuana kuwa mmoja wao kaoa/kaolewa; na wakaendelea na urafiki wao sioni tatizo. Kama ni dhambi watapambana na Mungu wao...Na mabinti wengine wala hawataki fyucha....ni migegedano tu kwa kwenda mbele na kula maisha ...
Na mitandaoni humu ni sandakarawe tu pata potea sawa na huko mitaani. Na kama tulivyoonywa sana na Mkwere kuwa humu "akili za kuambiwa ALWAYS changanya na zako".
Ila umetoa angalizo zuri Mama Mchungaji. Afadhali enzi zetu miaka ya 60 haya mambo ya mitandao hayakuwepo. Sasa ni vurugu tupu yaani. Poleni sana kwa kweli!
Juzi tu hapa jamaa yangu amegundua kuwa binti ambaye walikutana mtandaoni huko sijui twitter sijui wapi kumbe ni mke wa mtu na yeye keshampenda kabisa kabisa. Yaani mpaka anatia huruma kwa jinsi anavyohangaika...
Anyways niwatake radhi single men wote wa humu. Jamani tulianza kama utani kwamba wote humu mmeshaoa; coz sio kitu cha kweli. Personally nawafahamu vijana wengi tu huku ambao hawajaoa; so please ambao tumetishia "ndoano" zenu mtusamehe bure. Utani uliogeuka kuwa a serious talk along the way.
Kukumbushana ni muhimu kwa kweli hata kama hakuna under 10 humu. Yes kama nilivyosema kama umeoa/umeolewa au una mahusiano yako serious na umekutana na mtu na ukamtamani; mwambie tu ukweli ili ajue kusuka au kunyoa.
Kuna wanawake ambao wao naturally wanataka married men; so ukiwaambia ukweli wanakupokea kwa mikono miwili; they have nothing to lose. Au mwingine ajijue ni mchepuko akuchune kimahesabu au afanye makaretee ya kumpindua mkeo.
Kuna watu ambao wapo serious na wanahitaji mahusiano serious; hawana muda wa kupoteza. Huyu ukimdanganya kuwa hujaoa/olewa, akainvest kwako na kuachana na wote; afu baada ya miaka 2 ndiyo anakuja kushtukia kuwa umeoa/kuolewa aisee sio haki. Ni kumpotezea mtu muda na kumuharibia maisha yake. Imagine binti amebeba mimba ndiyo anagundua mwenzie ni mume wa mtu na katu hawezi kumuoa; anaishia kuwa singo mom na mtoto wa kufichwa juu.
Kuna binti December alikuja kulipiwa mahari; harusi ilikuwa soon after Easter. Vikao vimeshaanza kabisa; mara ghafla anapokea simu mtu anajitambulisha kama ni mke wa huyo mchumba wake. Akamtumia na copies za vyeti na picha za familia; kumbe mume alihamia kazi mkoa mwingine ndiyo kafika huko na kuwa MBA. Uchumba ikabidi uvunjwe; imagine how traumatized that lady is. Tusijitafutie laana zisizo na msingi
So tuwe tu wakweli; kuna kina Coca wao hawajali. Uwe tyuuu na ndinga siku mojamoja akanyage mafuta na kujisnap; muende hotels zenu n.k . Siku ukimuacha kwa raha zake anarudi zake kwenye daladala/mwendokasi kwa amani kabisa as anajua kuwa success isn't sexually transmitted. (coca nakutania mwanangu, usinichambe mama ako)





