Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it


Niliwahi kuingia nao kwenye taharuki mwaka 2016, yaani nipo sehemu nimekaa na washikaji kitaa mida saa tano asubuhi, tukashangaa ghafla defender imetia breki.

Kamanda wao akaamrisha tuingie kwenye gari kwa kosa la kunywa pombe ( bia) kabla ya muda ( enzi hizo haikuruhusiwa kunywa mpaka ifike saa kumi jioni). Nilishangaa sana maana tulikuwa tumekaa tu kumbe kuna tupu ( chupa) ya bia iko pembeni na sisi.

Wenzangu wakakubali kuingia mi nikakataa maana sikuwa na kosa, sijakaa sawa akaja mmoja eti anataka kunikamata, nikamdaka mkono na kimsukuma huko! Basi bhana sijakaa sawa wakaja wawili nikawadaka wote! Akarusha ngumi mmoja nikakwepa nikamrukia yule mwingine nikamtwisha hook punch.

Walikuwa kama nane hivi wengine walikuwa na chuma( SMG/ak 47).
Nikamvuta mmoja tena nikachana shati lake ( hakuvaa sare). Mzuka ukapanda niliwachezeshea mkono. Wale wenye bunduki wakakaa standby wakaniamuru nijisalimishe ( wala hawakuweka chamber risasi) nikawatukana.

Raia walijazana huku wakiwazomea hao polisi. Akaja mmoja tunafahamiana akaniomba niache. Akili ikarudi kuwa nimeharibu, nikapanda kwenye gari wakataka kuanza kunishambulia nikawaambia nitawavunjavunja na hizo silaha zenu ( wakatulia huku wamechakaa vumbi)

Tumefika kituoni nikaamuliwa kuvua mkanda ili niwekwe sero, nilipoutoa tu wakaanza mkanda huu umetoa wapi? Nikaawambia kwani unapatikana wapi?

Wakanywea; hahaha wakaniachia bure na knuckles wamekula.
Kwa komandoo lazima tu wangechemsha. Ila uliwaonea na kuwadhalilisha tu kwa sababu walikuwa kazini. Ungenena na bosi wao mambo yakaisha kistaarabu badala ya kuwatandika. Ila jamaa ni waonevu sana!
 
Kweli lakini kujitoa kote huko mwishowe unasikia hakuna kama mama.
Wazazi wote wana mchango mkubwa kwa mtoto ni vile mara nyingi mama ndo anayekuwa karibu na watoto tofauti na baba .

Kuna mdau aliweka uzi humu kuwa siku moja mwanae alimuomba hela ya kitu fulani akamnyima baadae yule mtoto akamuomba mama yake hela , mama yake akampatia yule mtoto hela bila kipingamizi , mtoto akafurahi mno baada ya kupewa kile anachohitaji .

Kwa scenario hii huyu mtoto atajua baba ukimuomba kitu hakupi ila mama yeye ukimuomba hapo hapo anakupatia , wakati mama anapewa hela na baba , wadau walishauri kuwa jamaa ampe hela mkewe mbele ya watoto ili waelewe hela inatoka baba kwa na sio mama .

Jambo kubwa na la msingi ni kwa wababa kuwa karibu na watoto zenu yaani muwe marafiki nao hapo itadumisha uhusiano mzuri kati ya baba na mtoto .
 
Una matatizo, na matatizo yako mimi tu ndie ninaeweza kuyamaliza!
Ombi
Babu yake, nikabidhi mjukuu wako ana matatizo mengi

Cc: Shimba Ya Buyenze

Mjukuu wangu bado mdogo sana. Mwache akue kue kwanza bana!

Kumbuka kuwa ladha ya tunda lililochumwa kabla halijaiva na lile lililoachwa likaivia mtini inatofautiana. Vumilia!
 
IMG_20220114_153345_048.jpg
 
Mjukuu wangu bado mdogo sana. Mwache akue kue kwanza bana!

Kumbuka kuwa ladha ya tunda lililochumwa kabla halijaiva na lile lililoachwa likaivia mtini inatofautiana. Vumilia!
We babu wewe, sasa nimuache akue vipi wakati mimi mwenyewe nina 27 si ndio nakuwa nae, kuhusu tunda ukiona halijaviwa kumbuka kuna wahuni wanalila na chumvi tena huko huko mtini!!
 
Hapana mdogo angu. Sio lazima kila mtu apitie magumu kwanza kwenye mahusiano ndiyo aje upate furaha. Wengine Mungu atawapa wa kuwadekea mapema sana.
The same to my late father...despite all his weaknesses but he was the best dad to me.
Kuna muda tulikwaruzana,,,
Mimi pia ni mpenda attention,,,sasa kwa baba yangu ni kama nilifika penyewe
Nikikaa nikikumbuka matukio mazuri(mf mzuri graduation yangu ya form four mzee alivyoinuka na kunipigia makofi nikiwa napewa zawadi zangu..ukumbi mzima walijua yule ni baba yangu)
Amenifunza appreciation..
Alikuwa akianza kukusifia na kukuelezea mzee wangu ahhh
Unaweza kulia kwa furaha.


Katika malezi yangu sikuwahi kupigwa na baba yangu hata siku moja.



Basi huku kwenye mahusiano mambo yatakuwa magumu,,,napenda care mno aisee...jinsi nilivyokuwa napiga stori na mzee...sijui km nitapata tena mtu wa aina ile maishani.
 
Mimi mama alikuwa anatoa maagizo kwamba ole wenu nikute mtoto analia.


Majuzi kati tu hapa nilipomaliza masomo,siku nimerudi nyumbani mama akasema tumtafutie mtoto kuku hata wawili,,ale..miaka yote aliyokuwa masomoni Mungu amemsaidia(walikuwa wanaona haiwezekani mimi kukaa mbali na nyumbani)

Baba akachinja kuku,mama akapika,anasema mtoto ale pekeyake..dada angu akasema"kwamba tumeanza kuchanganyikiwa tumuachie ale kuku wote pekeyake tunamuangalia tukwani ndio mara ya kwanza anarudi nyumbani?
.......
Hii favor sidhani kama nitakuja kuipata huko duniani.
Huyu kuku ht mi nisingekubali ule peke yako looh!
 
Couldn't agree more.
Umeandika vyema sana ,hongera kwa uandishi mzuri hivi .
Hakika upendo wa baba ni mkubwa sana kwa binti yake , natamani ningelelewa na baba muda wote ila hakuwezekana maana alienda kikazi mkoa akaja kurudi tayari nimefikia umri wa miaka 12 .

Hii ikatufanya tumuogope maana alkuwa mkali sana , ikatokea hadi tukajiweka mbali naye na kuwa watoto wa mama tu , ila Mungu huyu baadaye Mama akafariki , tulilalamika sana kwa nini mama hayupo lakini Mungu alikuwa na sababu kubwa na leo hii tumejua kuwa baba ni mtu peace sana .

Kiukweli bila upendo wa baba maisha hayaendi maana utaanza kutafuta upendo nje ambapo utakutana na watu wasiofaa , kitu kikubwa ambacho wazazi wanachotakiwa kufanya ni kuweka mawasiliano ya karibu na watoto .
 
Kuna kitu nilikuwa nawaandikia na Saint Anne hapa. Hakuna kitu kimenijenga na kunisaidia sana katika maisha yangu kama mahusiano mazuri na baba yangu. His love, care, attention, protection and everything he gave to me; vimenipa kujiamini, kujipenda, kujithamini na of coz kuwa na upendo mwingine sana kwa wengine.

Nilipata changamoto kidogo wakati naanza dating; i thought all men are just kike my father; so nilitegemea care, attention na makila kitu; ila slowly wakanifundisha kuwa wao sio baba zangu (msicheke). Na my greatest weakness ni kupenda attention; hiyo ni mpaka kesho kutwa. So kiugumuugumu nikaanza kupunguza madeko hadi ukimpata wa kukudekesha.

Ila katika yote; binti aliyelelewa kwa upendo na baba yake; ni binti anaye-value wanaume sana. Pamoja na vitu vizito vyote vilivyonipiga huko; sikuwahi kuwachukia wanaume wala kubeba uchungu juu yao wala kugive up kwenye mapenzi. Huwa naamini wanaume wazuri wapo wengi tu. So utakuwa mvumilivu hadi siku charming prince anapootokea

Binti aliyependwa na baba yake; anakuwa mvumilivu ila hawezi kusettle kwenye abusive relationship. Anajua nini maana ya kupendwa, so there is no way ataona sawa kukaa kwenye sehemu ambayo hapendwi na anaumizwa kimwili au kihisia. So sio rahisi kufa kisa ndoa.

Too bad nilikuja kukutana na a certain case ya sexual abuse kwa mabinti kadhaa; too bad wote walikuwa na dad issues. Karibu wote wana absentee fathers au wale waliobahatika kukaa nao, ni wale kina baba wa kutoa matumizi basi. Mabinti wa hivi wanakuwa vulnerable to sexual abuse; kuna watu wanaweza kuwa-manipulate wakijifanya wanawapenda lakini wanawatumia. Ni kama wana kiu ya kupendwa so wakikutana na manipulators, wanatake advantage. Mtu ambaye ameshaonyeshwa upendo wa kutosha huwezi kumdanganya tu na vi -i love you afu eti ukamtumia; they know and have seen what i love you means. Baba akiwepo, ukitugusa tu au ukitusumbua, tumeshaenda kusema; so hata kuwa abused si rahisi

Mama mchungaji wangu kuna siku alituambia " ni heri kumkosa mama kuliko baba". Kila mwanamke ana umama ndani yake; so ukimpoteza mama kuna aunt, kuna dada, kuna ma mdogo, bibi n.k wanaweza wakakulea kama mama. Lakini sio kila mwanaume ana ubaba ndani yake; so ukibahatika kumpata mwanaume mwenye ubaba halafu ukampoteza; aisee ni umepoteza haswa. Mwisho wa kunukuu.
This is me...!!!binamu hua hukosei una akili sana!Fanya baasi tuonane!
 
Back
Top Bottom