[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119]
Niliwahi kuingia nao kwenye taharuki mwaka 2016, yaani nipo sehemu nimekaa na washikaji kitaa mida saa tano asubuhi, tukashangaa ghafla defender imetia breki.
Kamanda wao akaamrisha tuingie kwenye gari kwa kosa la kunywa pombe ( bia) kabla ya muda ( enzi hizo haikuruhusiwa kunywa mpaka ifike saa kumi jioni). Nilishangaa sana maana tulikuwa tumekaa tu kumbe kuna tupu ( chupa) ya bia iko pembeni na sisi.
Wenzangu wakakubali kuingia mi nikakataa maana sikuwa na kosa, sijakaa sawa akaja mmoja eti anataka kunikamata, nikamdaka mkono na kimsukuma huko! Basi bhana sijakaa sawa wakaja wawili nikawadaka wote! Akarusha ngumi mmoja nikakwepa nikamrukia yule mwingine nikamtwisha hook punch.
Walikuwa kama nane hivi wengine walikuwa na chuma( SMG/ak 47).
Nikamvuta mmoja tena nikachana shati lake ( hakuvaa sare). Mzuka ukapanda niliwachezeshea mkono. Wale wenye bunduki wakakaa standby wakaniamuru nijisalimishe ( wala hawakuweka chamber risasi) nikawatukana.
Raia walijazana huku wakiwazomea hao polisi. Akaja mmoja tunafahamiana akaniomba niache. Akili ikarudi kuwa nimeharibu, nikapanda kwenye gari wakataka kuanza kunishambulia nikawaambia nitawavunjavunja na hizo silaha zenu ( wakatulia huku wamechakaa vumbi)
Tumefika kituoni nikaamuliwa kuvua mkanda ili niwekwe sero, nilipoutoa tu wakaanza mkanda huu umetoa wapi? Nikaawambia kwani unapatikana wapi?
Wakanywea; hahaha wakaniachia bure na knuckles wamekula.
Ulifanya la maana kamanda. Hawa viumbe wengi wao wana vurugu na ni waonevu sana ukiwa mnyonge utaonewa sana.
Kuna scenario moja ilitokea maeneo fulani. Kuna traffic polisi wale wanawaitaga tigo sijui voda fasta wale ambao wakikuambia usimamishe gari ukakimbia wanakufukuzia na vile vipikipiki vyao hadi wakukamate.
Basi bhana kuna siku wakamsimamsha jamaa mmoja jamaa akaona pale aliposimamishwa hakuna sehemu nzuri ya kupaki hivyo akasogea mbele kidogo ili apaki. Wale jamaa wakajua labda sijui anakimbia wakaanza kumfukuzia alipofika akapaki ile anashuka tu wakaanza kumshambulia oo we kwanini tunakuambia usimame unakimbia.
Jamaa hata hajapata nafasi ya kujielezea wakaanza kumtia mateke mara mitama jamaa akawa tu mpole wala hakutaka kusema yeye ni nani. Tena alikuwa amevalia koti jeupe la kidaktari wakamvua wakalitupa chini wakaendelea kumpiga.
Pembeni kulikuwa na kituo cha bodaboda. Wale bodaboda wengi wao walikuwa wanamjua jamaa aliyepigwa ni nani. Basi kwa pembeni wakaanza kuambizana kuwa hivi hawa polisi wanajua wanayempiga ni nani hawajui kama ni boss huyo.
Wale polisi wakasikia yale maneno ya bodaboda wakawa kama wamepunguza kumpiga wakabaki wanajiuliza huyu atakuwa nani mbona hawa bodaboda wanasema hivyo. Wakati wale mapolisi wanaendelea kushangaa yule jamaa akapata nafasi akapiga simu Lugalo kumbe jamaa ni daktari pale Lugalo.
Ndani ya dakika chache tu ilitoka defender Lugalo imejaa ma MP. Wale matraffic wakawa bado wamezubaa tu hawajui kinachoendelea pale pale wakapakizwa kwenye defender wakapelekwa Lugalo.
Sasa wakati wanapakizwa wale bodaboda wakawa wanashangilia wanasema ndiyo wakamateni hao wamempiga boss wetu ona wamemtupia hadi koti lake wamemchafulia. Inaonesha wale bodaboda nao walikuwa hawawapendi wale matraffic na walishawachoka na tabia zao za uonevu.
Polisi wetu (wengi wao) inabidi wajitafakari sana asee hawajiulizi kwanini kila kukicha wanalalamikiwa wao tu yaani hiyo tabia yao ya uonevu wananchi wengi wameshaichoka. Huwa najisemea tu sasa huyo kwa vile alikuwa ni mwanajeshi ndiyo maana wale mapolisi ilikula kwao.
Jiulize ni raia wangapi wanaonewa na kuteswa kama hivyo huko mitaani kwa sababu tu hawana mamlaka yoyote. Ni wengi sana sema tu ni vile hawana cha kujitetea wala pa kusemea.
Watu wanaleta uonevu hadi kwa watu wasiowajua halafu yakiwakuta ya kuwakuta wanaanza kusema wanajeshi wakorofi na wana roho mbaya. Wacha waendelee kujichanganya na kuingia kwenye anga za watu wasiowajua.