Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Wakuu.

Japo hatujuani lakini tunaishi kama ndugu. Na hakuna kitu cha thamani kama kuombewa na kutakiwa mema na mtu usiyemfahamu. Maombi ya aina hii huwa na nguvu sana kwa sababu huwa ni maombi ya kweli yasiyo na ajenda wala mawaa.

Napenda nichukue nafasi hii kuwashukuru wote mlioniombea na kunitakia mema; na uponaji wa haraka. Japo Covid hii (tena Delta mwenyewe) ilinijia kwa nguvu sana lakini kwa maombi yenu na upendo wa Mungu nimepona. Bado tu kakikohozi ka mbali lakini hata nikikimbia kifua hakiwaki moto kama hapo kabla...na viuchovu uchovu tu vya hapa na pale. Kwa jina la Yesu naamini kuwa nimeshapona

Sikuweza kumjibu mmoja mmoja lakini kwa umoja wenu napenda sana kuwashukuru mno 9.8ms squared, Heaven Sent, mahondaw, Makiwendo, Saint Anne, T 1990 ELY, Tinsley, Gregory 2000, Karma, Kashaija72, Chakorii na mawardat.

Asanteni sana wapendwa na Mungu Awalinde na kuwabariki sana. Hapa nilipo ni kama naishi peke yangu lakini kupitia kwenu nilijiona kama nina jeshi kubwa la watu wanaoniombea na kunitakia mema.

Hebu Mungu Akatubariki sote na mwaka huu mpya ulioanza ukawe wa mibaraka tele; na kila mmoja wetu akaweze kutimiza ndoto zake na malengo aliyojiwekea.

Nawashukuru sana


View attachment 2075249
Amen
 
Jua la jioni,,,,mchanga wa GMZ
IMG_20220111_173623.jpg
 
Inaweza ikawa kweli au sio kweli pia. Leo kuna watu wengi tu ambao wameinuliwa na marafiki zao, wakati ndugu zao walikuwa na uwezo wa kuwasaidia and yet waliwatelekeza. Mungu akikujaalia ukampata rafiki mwema; unakuwa umejipatia kitu chema sana.
Imenitokea mimi kupewa connection Na rafiki nikatoboa Na ndugu yangu niliyemwamini akanipiga chini.Wacheni Mungu aitwe Mungu.kwenye maisha yangu yote ya hapa duniania nitakuwa natoa Kwa wahitaji 💯
 
Back
Top Bottom