Ilikuwa alfajiri ya jumapili
Bwana Yesu alipoyashinda mauti
Kamba za kuzimu zilimwachia
Haleluya wokovu ni thabiti
Mwanakondoo kaondoa dhambi
Wala hakuna alilolisaza
Deni zetu zote amezilipa
Kwa damu.
Basi utwae uzima kwa kufurahi
Upokee kwa Bwana sasa
Ujijue hakika kwake utaishi
Bwana Yesu ameshafufuka
Yesu katoa uzima wa bure
Autakaye apokea bure
Ili aishi naye kule Mbinguni
Mileleee