Watu wanaenda kanisa kama tamaduni mkuu. Mtu hawezi kuwa anafurahi juu ya dhambi flani au kuisifia nikamuunga mkono ni sawa na kushiriki dhambi zake.. kitu ambacho hakina afya kwa nafsi yangu na roho yangu.
Walokole wengi (hata wale feki) huwa wanajiona kama wana hatimiliki na Mungu; na wana ka authority fulani hivi na Neno lake. Ila ukiangalia maneno na matendo yao sasa mpaka unatikisa kichwa.
Kila mtu na ashike sana alichonacho hasa nyakati hizi ambapo watu hawaogopi kitu tena; mpaka dhambi za kinyama zinatendeka mchana peupe; huku zikitetewa na kuungwa mkono waziwazi na hata kupigiwa kampeni. Dhambi inapigiwa kampeni!
Dunia nzima sasa imejifunga kibwebwe kueneza na kusambaza ushoga. Huwezi kuangalia muvi kwa amani bila kukutana na ushoga. Mpaka katuni za watoto. Wanataka wawakamate tangu wakiwa wadogo ili wazoee na kuona ushoga kuwa ni jambo la kawaida tu tena la kifahari! Na kama unataka uharibu career yako jaribu tu kuusema ushoga vibaya. Utafukuzwa kazi na kuandamwa sana. Utaitwa homophobic. Intolerant. Mtu wa hatari usiyefaa! Mpaka imekuwa kama sifa fulani hivi mtu akijitangaza kuwa ni shoga (ku- come out). Anaye-come out ndo ataitwa shujaa na mwenye courage. Shujaa wa nini? Courage ipi? Wanajua wenyewe!
Kwa nini dunia nzima inapiga kampeni ku promote ushoga? Kuna kitu gani ambacho ni so special kuhusu ushoga? Kwa nini siyo dhambi zingine? Wapo wanathiolojia ya unabii wanaofungamanisha kampeni hizi na mfumo mzima wa kumwondoa binadamu na kumtenga mbali kabisa na Mungu lengo likiwa ni kuweka mazingira mazuri ya New World Order - serikali moja ambayo kiongozi wake mkuu atakuwa ni yule mpinga kristo aliyetabiriwa kuwa atatokea siku za mwisho kabla ya Masihi kurudi. Eti huyo mpinga Kristo naye atakuwa shoga! Kwamba, japo dhambi zote ni machukizo kwa Mungu na mshahara wake ni mauti, hakuna dhambi yenye kudhalilisha utu na kumfikisha binadamu katika utengano kamili na Mungu wake kama ushoga. Ndiyo maana dunia imewekeza sana katika dhambi hii na waalimu wa unabii wanasema kuwa haijawahi kutokea dunia nzima kuungana katika kupromote dhambi kuu waziwazi namna hii kama tunavyoshuhudia leo.
Mnaweza kukesha hapa mkibishana na kutukanana lakini wenye dunia yao wanajua kinachoendelea ndiyo maana wamewekeza mabilioni ya dola kwenye ajenda hii. Na kama ilivyokuwa kwenye suala la demokrasia (vyama vingi), inaaminika kuwa ushoga nao utalazimishwa tu kama ajenda ya jumla kwa mataifa yote duniani. Usiporuhusu ushoga unanyimwa misaada ya kiuchumi na wakubwa wa dunia. Unatengwa! Na ushoga sasa ni suala la haki za msingi za kibinadamu! Unaweza kupiga marufuku ulevi, uzinzi na dhambi zingine zote hakuna atakayejali. Lakini gusa ushoga sasa uone! Dunia nzima itakumulika. Na utasalimu amri tu!
Basi kila mtu na ashike sana alichonacho! [emoji2221][emoji2221][emoji2221][emoji2221][emoji2221]