Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Huyo Mungu wako asie na mizani namkataa ha ha haaWote motoni sawa ila je kwa kipimo kimoja au kuna atakaemzidi mwenzie moto?
Hivyo vipimo sasa jitahidi leo ufanye maombi umuulize Mungu vipimo vyake mkuu.
 
Hayo nayo yakatae tu.Kutamka hilo neno hadharani siwezi.

Ila mlevi linatamkika hata kwa watoto shangaa hapo tetea tu ila usilinganishe uzito wake.
Kwani wapi tumeyakubali mkuu?
Hebu onyesha tulipoyakubali sasahivi ili tuyakatae.
 
Shida ni hutumii tafsida dogo.. Ukiandika ushoga wala haishtui kuliko ilo neno unaloandika
Hata aliyeniquote aliandika hivyohivyo.
Mimi nimeflow tu vilevile.


Pia kiswahili nadhani nilikuwa mbovu darasani.
 
Hivi Saint Anne hakukuambia wewe kwamba kipindi ndiyo anaingia kwenye huu uzi tulivyojua ni shoga tulimshambulia na wala hakuna aliyemtetea? Na hata leo hii pia hakuna anayemtetea ila tunachosema ni kwamba tu tuache unafiki kuchagua dhambi za kuwaambia watu waache au waendelee!

Binafsi roho huwa inanisuta watu wanaposambaza video zao za ngono na wengine hatukemei tena ndiyo kwanza tunashangilia na kuomba tutumiane hata pm! Lakini mtu kuuongelea tu ushoga hajatuma video yoyote inayoonesha ila watu tunamtukana kama vile sisi ndiyo watakatifu sana!

Vizuri kama umejitafakari kuhusu ulevi kwa sababu hata mimi ni mlevi lakini sifurahii hii dhambi na wala siwezi kujiona bora sana kuliko shoga! Mimi napenda mtu akemee kila dhambi siyo anakemea dhambi moja halafu nyingine anaichekelea na tunaokemewa nasi tujitafakari tutubu na tujitahidi tuache!
Hivi ana uhakika gani kuwa huyu dogo hakatazwi?
Hajui huyu dogo ground analimwa semina za maana kuhusu hayo,,au kila akilimwa semina itangazwe humu kuwa sasa tupo kuimbisha dogo injili.
 
Lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika. + Bali wewe ukue katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao, + na yakuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. +(2Tim 3:13-15)
 
Teh mkuu wewe ndiyo ulinisingizia kuwa mimi natetea ushoga au umesahau sasa kati ya mimi na wewe nani mnaa? Wewe umenipa maandiko kutoka kwenye biblia nami nimekupa andiko kutoka kwenye biblia ila cha ajabu nikikupa mimi unapinga ila ukinipa wewe unataka nikubali as if ninayokupa mimi natunga mwenyewe!

Kuna comment kule juu nilikuuliza shoga akitubu anaenda mbinguni au haendi ukanijibu anaenda na ukakubali kwamba hata naye anasamehewa kama wengine hadi ukaingiza sijui habari za TPDF na kunitaka nikemee ushoga! Sasa kwanini tuzunguke sana ikiwa shoga naye akitubu ataenda mbinguni kama ambavyo mzinzi naye akitubu ataenda?

Mimi nilikupa maandiko haya:

Luka 6: 42
Au, utawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huiangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi kilichomo katika jicho la ndugu yako.

1 Wakorintho 6: 9 - 10
9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,

10 wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi.

1 Wakorintho 6: 18 - 20
18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.

19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;

20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

Mwanzo ulikuwa unarukaruka ila baada ya kulipata hilo andiko moja ndiyo umeamua ushikilie hapo hapo ukifikiri kwamba hilo andiko ndiyo litafunika hayo maandiko mengine yote! Unafikiri hilo andiko la ufunuo ulilokazania ndiyo linapinga hayo maandiko mengine yote?

Hakuna sehemu biblia inasema adhabu ya moto itatofautiana kulingana na dhambi alizotenda mtu! Labda unioneshe ni wapi biblia inasema kuna levels za ukali wa moto wa jehanam kulingana na ukubwa wa dhambi nioneshe!

Mkuu wewe ndiyo hujui kuchambua biblia ndiyo maana ukatoa mifano kama eti sijui kwanini Lutu alipokuwa anakunywa pombe na kufanya mapenzi na wanawe ule moto wa Sodoma na Gomora haukuja kuwaunguza na wao duuh! Haki nilicheka na kushangaa sana siku ile!

Na inaonesha hata Mungu mwenyewe bado hujamjua vizuri namna anavyofanya kazi zake achilia mbali hayo maandiko yake! Sema kwa vile nimekaa kimya kuhusu hayo mkuu wangu basi ndiyo ukajiona unajua kuchambua hayo maandiko kuliko hata wale waliyoyaandika mwee na kuwaona wengine hawajui kitu!

Kwahiyo mimi kukalia kimya baadhi ya mambo ambayo naona kabisa hauyajui na umepuyanga haikufanyi uwe sahihi katika hayo yote unayoandika! Ila wewe naona umekazana kusema tu nimeshindwa sijui wewe ndiyo mshindi sasa sijui ni mashindano gani hayo ambayo umeshinda dooh pathetic!

Na naona unafikiri kwamba mimi kufunga huu mjadala basi ndiyo nimeshindwa kuendelea kukuelewesha au eti nimekubaliana na wewe kwa kila ulichoandika! Maana naona unanilazimisha kweli nikubaliane na wewe tofauti na mimi ninayekuelewesha taratibu na kukuacha ujitafakari ili ukitaka uyachukue usipotaka uyaache kiroho safi tu!

Niliamua kufunga mjadala ili niokoe muda wangu na nguvu zangu maana nimeshaona hapa hatutafika mwisho wala kufikia suluhisho halafu sifaidiki na chochote! Mimi ninapoquote wengine wala sijakutaja wewe ila umejihisi tu mimi nimeamua kukuacha ubaki na imani yako na mimi nibaki na imani yangu ila kama utataka kuendelea kujitunuku huo ushindi hewa basi endelea tu mkuu the floor is all yours mie huo utoto siuwezi so nimeshamalizana na wewe kuhusu habari za ushoga na hayo maandiko usiyojua tafsiri yake!
Anafikiri umechoka?
Akasome ule uzi wa Nyenyere wa mwaka juzi
 
Uhuru day
20211209_162431.jpg
 
Back
Top Bottom