Nimegundua kinachowaponza wanaume wengi ni kukariri maisha! Kwamba hakuna mwanamke anayeweza kuvumilia shida kwa muda mrefu!
Kuna jamaa alifanya huo huo mchezo kama wa bro wako! Anatafuta mwanamke wa kuoa akashauriana na washikaji zake kwamba akipata mchumba afiche mali zake zote ajifanye masikini ili ampime!
Kweli alipata mchumba yule dada alikuwa na maisha ya kawaida tu muajiriwa ana kamshahara kake ka kawaida tu kapanga vyumba viwili maisha yanasonga. Jamaa alikuwa na majumba na magari mengine ya urithi.
Basi wakaanza mahusiano dada siku zote anajua mpenzi wake ni masikini anafanya kazi za saidia fundi anaishi kwenye kaghetto tu. Ila alimpenda na alimheshimu hivyo hivyo na siku zote alikuwa willing kumsaidia na hakuwahi lalamika.
Imepita miezi sita jamaa na washikaji zake wameshajiridhisha wakakubaliana kwamba hapa sasa mke kapatikana. Cha msingi amuambie ukweli wote na nia yake ya kufanya vile kisha ampropose amvishe pete na mchakato wa ndoa uanze.
Kweli wakapanga mfanyia surprise siku ya siku wameandaa bonge la party kwa ajili ya proposal tu tumia gharama nyingi sana ita ndugu na jamaa kama wote. Mdada kufika pale anaona hali haielewielewi ghafla anamuona bwana wake kavaa kidon don halafu mambo ya kifahari kama yote nini.
Jamaa kabla ya zoezi la kuvisha pete ikabidi aanze kujielezea kwanza kuwa oo sijui unajua mimi siko kama nilivyojitambulisha kwako nilifanya vile ili sijui nipate mke mwenye mapenzi ya kweli blah blah kikaenda kikarudi kikapanda kikashuka. Wakajua mchumba atafurahia na mapenzi ndiyo yataongezeka maradufu.
Cha ajabu walishangaa yule dada alichukia na bila kujibu kitu pale pale akaondoka watu wanashangaa kulikoni ikabidi waanze kumfukuzia wakamkosa na sherehe ikaishia hapo. Baadaye jamaa kumtafuta kwenye simu akaomba wakutane amueleze kwanini alifanya vile dada akaanza kufunguka.
Oo unajua mimi maishani mwangu sikuwahi tamani kuwa na mwanaume mwenye pesa hasa ambaye nimemkuta nazo kwa sababu wanaume wenye pesa huwa hawana mapenzi ya kweli. Wengi wahuni na wanamchukulia mwanamke kama chombo cha starehe tu na hata wakioa wanaoa kama geresha tu ila huko nje kuna kuwa na msururu wa wanawake na wote kawazalisha.
Akamuambia mimi nilikupenda sababu ya umasikini wako na nilidhani wewe ni masikini kweli na nilikuwa tayari mimi na wewe tuanze wote from the scratch. Ili mwisho wa siku usije ukaanza kunidharau na kusema kwamba sina msaada kwako maana nimekukuta una kila kitu.
Basi ndiyo mapenzi yakawa yameishia hapo na yule dada alikuwa serious kabisa jamaa hakuamini. Halafu ukicheck jamaa alikuwa kafa kaoza maana alikuwa ashahitimisha zoezi la kutafuta mke akijua sasa hapo kinachosubiriwa ni ndoa tu kwa wakati huo hakuna mwanamke aliyekuwa anampenda kama huyo japo alikuwa na vimichepuko kama vyote.
Lakini vile vimichepuko vilikuwa ni vya kupiga na kusepa tu maana alishajua vimempendea pesa zake ila huyu mama la mama ndiye alikuwa kwenye plans zake sema ndiyo hivyo tena. Basi jamaa jitetea jitetea na wewe omba msamaha sana ila wapi ndiyo ikawa imeisha hiyo hadi leo anaumia na hajaoa.
Kwahiyo msikariri kwamba wanawake wote wanapenda wanaume wenye pesa tu wengine wanahitaji mapenzi ya kweli tu pesa mtatafuta wote. Maana wanawake wengi tunajua kuwa pesa na mapenzi ya kweli havishabihiani hivyo kuna wataochagua mapenzi ya kweli na kuna wale wenzangu na mimi waliokunywa uji wa wagonjwa wao ni pesa 'mbere' mapenzi ya kweli bakini nayo watayapata mbinguni kwa baba.
Ila dunia hii yaani hata mimi nilipigwa na butwaa kiukweli nilidhani nimeshasikia yote hadi nilipokuja kusimuliwa hicho kisa na aliyenisimulia ni rafiki yangu ambaye aliujua mchezo mzima na alikuwepo kwenye hiyo party ni ndugu wa huyo jamaa! Ila daah siku hizi mapenzi hakuna aisee hata hao wanaume masikini wenyewe nao wana misururu traffic anasubiri acheni tu wanawake waangalie mifuko jamani maana hayo mapenzi ya kweli hayako tena kila mtu msaliti!
Good story😊 halafu sasa unalivyoandika ni kama unahadithia kwa mdomo😁, we inaonekana ni mpiga story mzuri😊..
Niongee tu ukweli, wanasema msema 'kweri' ni mpenzi wa mungu..
Wanawake wengi hawapo kama huyo dada, naye itakuwa alikuwa hivyo baada ya kuumizwa sana na mtu ambae alimpenda kwa dhati na akamtenda, akaapa kutokuja kuwa na mahusiano na mtu wa aina hio, lakini alikosea ku generalize..
Lakini ukweli ni kwamba wanawake unaweza muuliza mwanaume amekuletea zawadi gani wakati ametoka jela, sio wote lakini majority..
women dont care about us , that is the way it is at the end, sio kwamba nawachukia no! nisieleweke vibaya, at the end of the day, they only care about themselves. they care about their own needs being met, they only care about what you can do for them, you are almost like entertainer, you have to keep her happy at all times, its all abt her,.... najua its hard pill to shallow, hii ni part ya female nature na huo ndio ukweli... so siwachukii
specificly they care abt what you can do for them and what you are doing for her, wanachojali ni value unayompatia sasa whether it be financial value, you might be taking care of the kids while she's at work, you might be giving her sexual glatification, yaani in general you are providing some value in her life to where you are keeping her around..
unaweza pigwa chini kwa higher value male anytime, thats how it works, kama kuna wanao argue ukifikiri nguvu za kiume and all that utapendwa zaidi , ukifikiri she can love you unconditionally, then nenda kafanye hivyo unavyohisi ukifanya utapendwa saana and see how it turns out😂
i'm aware of female nature, i do not live my life for them, i live my life for me, i live my life on my terms.😊
Niseme tena sio wote Ila majority almost 95% wapo hivyo, na hio ni nature, so kuna wachache ambao dhahabu, na ili dhahabu pure ijulikane lazima ipite kwenye Moto..
Wanawake walio after s'thing siwachukii nirudie tena, that's why mwanzoni nilisema uki date na mtu akanambia una pesa kiasi gani? Unaweza kuni afford?, siwezi mchukia na nikasema ni gold digger, huyo nitamjibu vizuri tu kama nitamu afford au la, cause at the end ni part ya female nature..😊
Kwa hio Karma wewe kuzungumza haya maneno ni kutetea kwa mifano ambayo ipo na ni michache lakini majority hawapo hivyo..
Wanaume wenzangu wananielewa..
Watakaokupenda unconditionally wapo ndio hao sasa kufahamu japo it's not guarantee, chujio la chuma lazima lipite..
Kuna story moja ya star Fulani kuhusu alichofanyiwa na mkewe inasikitisha sana, I think ni Mabeste.. unaweza rejea hio story..