Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Nina software ina analyse sura yako hata kama ni side-view, inaweza jua gender, emotions, age n.k, inafanya geometric proportions ya sura yako na kuleta sura yako ilivyo

Pia inatoa beauty score kwa rate ya 1-100%, na hapa naona inanipa 100%, ni kitu ambacho haijwahi nipa score ya namna hio..😉

Ipo accurately, ni mambo ya AI na machine learning 😊

Au nikuoneshe sura yako hapa hapa?
 
Haiwezekani. Huwezi ukawa umesahau ule uzazi wako wa mwisho. Usije tu ukanisumbulia mkono wangu, yakikukuta
Screenshot_20211026-235056.jpg
 
Nina software ina analyse sura yako hata kama ni side-view, inaweza jua gender, emotions, age n.k, inafanya geometric proportions ya sura yako na kuleta sura yako ilivyo

Pia inatoa beauty score kwa rate ya 1-100%, na hapa naona inanipa 100%, ni kitu ambacho haijwahi nipa score ya namna hio..😉

Ipo accurately, ni mambo ya AI na machine learning 😊

Au nikuoneshe sura yako hapa hapa?
☺☺☺ sio kwa kunipamba huko. 😉

Hiyo software mbona kama inaongeza chumvi nyingi sana jamani??? Nitumie nijihakikishie kabla kichwa hakijajaa 😁🙈🙈

Haya tuma picha tuone please 🙂
 
My brother alipata mchumba, dada mmoja asili ya ki Asia, nilichoandika hapo mkuu tuliki practice in real life nakupa true story kabisa..

Jamaa ndiye alileta wazo kwa sababu anataka kumuoa huyo binti baada ya mahusiano ya uchumba..

Akanishirikisha nikamwambia haina shida ni wewe tu..

Jamaa akanikabidhi funguo za gari zake 2, akamficha mchumba wake kuhusiana na status halisi aliyokuwa nayo, alimwambia gari ameuza kulipa madeni..

Walikwenda kupanga uswahilini, yule dada alikuwaga amezoea ku drive akaanza kupewa nauli kwenda chuoni, at the time alikuwa mwanafunzi anajiendeleza..

Dada kapambana sana na daladala, akirudi maskani ni hadithi za vituko vya kwenye daladala, basi bwana ukapita mwezi, jamaa alikuja kunieleza kwamba imetosha anaona kafaulu tayari, nikamwambia pambana na hali yako, funguo sikupi tumekubaliana miezi mitatu we mwezi mmoja tu unaanza kubadili mawazo, jamaa akanambia anamuonea sana huruma..

Mzee wa kushauri nilikuwa nimesimamia msimamo wangu, nikamwambia sasa anza na kumuomba pesa kabisa, mwambie upo broke mbaya

Jamaa akasafiri kwenda mkoa flani kikazi, huko akawa anampigia mchumba wake simu kwamba hali ni mbaya, hana pesa ya kula, dada anatuma pesa, jamaa anamuuliza umeiotoa wapi? anasema mama alinipatia nikatunza..

Life likasonga, mwezi wa pili, mwezi wa 3, binti alifaulu ule mtihani hata mie sikuamini kabisa, niliweka msimamo kwa sababu huyu msichana nishazinguana nae, angefeli ingekuwa fresh tu kwangu.., angefaulu pia ingekua fresh cause bro angekuwa amepata mwanamke sahihi..

Nilimkabidhi jamaa funguo zake akiwa na furaha kinoma, ndoa ilifungwa wiki chache baadae, siku hio nilicheza mziki ukumbini mpaka watu walinishangaa..

Na mie nilijipiga siku hio nikawapatia zawadi ya fridge, ngoja niangalie picha kama ipo kipindi natoa zawadi niiweke..

Basi ikawa hivyo, jamaa alinushukuru baadae, wakawa mke na mme..

Mi sio mwandishi mzuri..

Mkuu hii sio hot tea, hii kitu imenitokea na nimei practice kabisa..

Wapo kwenye ndoa miaka michache sasa, wana 2 beautiful daughters na life linasonga..
Nimegundua kinachowaponza wanaume wengi ni kukariri maisha! Kwamba hakuna mwanamke anayeweza kuvumilia shida kwa muda mrefu!

Kuna jamaa alifanya huo huo mchezo kama wa bro wako! Anatafuta mwanamke wa kuoa akashauriana na washikaji zake kwamba akipata mchumba afiche mali zake zote ajifanye masikini ili ampime!

Kweli alipata mchumba yule dada alikuwa na maisha ya kawaida tu muajiriwa ana kamshahara kake ka kawaida tu kapanga vyumba viwili maisha yanasonga. Jamaa alikuwa na majumba na magari mengine ya urithi.

Basi wakaanza mahusiano dada siku zote anajua mpenzi wake ni masikini anafanya kazi za saidia fundi anaishi kwenye kaghetto tu. Ila alimpenda na alimheshimu hivyo hivyo na siku zote alikuwa willing kumsaidia na hakuwahi lalamika.

Imepita miezi sita jamaa na washikaji zake wameshajiridhisha wakakubaliana kwamba hapa sasa mke kapatikana. Cha msingi amuambie ukweli wote na nia yake ya kufanya vile kisha ampropose amvishe pete na mchakato wa ndoa uanze.

Kweli wakapanga mfanyia surprise siku ya siku wameandaa bonge la party kwa ajili ya proposal tu tumia gharama nyingi sana ita ndugu na jamaa kama wote. Mdada kufika pale anaona hali haielewielewi ghafla anamuona bwana wake kavaa kidon don halafu mambo ya kifahari kama yote nini.

Jamaa kabla ya zoezi la kuvisha pete ikabidi aanze kujielezea kwanza kuwa oo sijui unajua mimi siko kama nilivyojitambulisha kwako nilifanya vile ili sijui nipate mke mwenye mapenzi ya kweli blah blah kikaenda kikarudi kikapanda kikashuka. Wakajua mchumba atafurahia na mapenzi ndiyo yataongezeka maradufu.

Cha ajabu walishangaa yule dada alichukia na bila kujibu kitu pale pale akaondoka watu wanashangaa kulikoni ikabidi waanze kumfukuzia wakamkosa na sherehe ikaishia hapo. Baadaye jamaa kumtafuta kwenye simu akaomba wakutane amueleze kwanini alifanya vile dada akaanza kufunguka.

Oo unajua mimi maishani mwangu sikuwahi tamani kuwa na mwanaume mwenye pesa hasa ambaye nimemkuta nazo kwa sababu wanaume wenye pesa huwa hawana mapenzi ya kweli. Wengi wahuni na wanamchukulia mwanamke kama chombo cha starehe tu na hata wakioa wanaoa kama geresha tu ila huko nje kuna kuwa na msururu wa wanawake na wote kawazalisha.

Akamuambia mimi nilikupenda sababu ya umasikini wako na nilidhani wewe ni masikini kweli na nilikuwa tayari mimi na wewe tuanze wote from the scratch. Ili mwisho wa siku usije ukaanza kunidharau na kusema kwamba sina msaada kwako maana nimekukuta una kila kitu.

Basi ndiyo mapenzi yakawa yameishia hapo na yule dada alikuwa serious kabisa jamaa hakuamini. Halafu ukicheck jamaa alikuwa kafa kaoza maana alikuwa ashahitimisha zoezi la kutafuta mke akijua sasa hapo kinachosubiriwa ni ndoa tu kwa wakati huo hakuna mwanamke aliyekuwa anampenda kama huyo japo alikuwa na vimichepuko kama vyote.

Lakini vile vimichepuko vilikuwa ni vya kupiga na kusepa tu maana alishajua vimempendea pesa zake ila huyu mama la mama ndiye alikuwa kwenye plans zake sema ndiyo hivyo tena. Basi jamaa jitetea jitetea na wewe omba msamaha sana ila wapi ndiyo ikawa imeisha hiyo hadi leo anaumia na hajaoa.

Kwahiyo msikariri kwamba wanawake wote wanapenda wanaume wenye pesa tu wengine wanahitaji mapenzi ya kweli tu pesa mtatafuta wote. Maana wanawake wengi tunajua kuwa pesa na mapenzi ya kweli havishabihiani hivyo kuna wataochagua mapenzi ya kweli na kuna wale wenzangu na mimi waliokunywa uji wa wagonjwa wao ni pesa 'mbere' mapenzi ya kweli bakini nayo watayapata mbinguni kwa baba.

Ila dunia hii yaani hata mimi nilipigwa na butwaa kiukweli nilidhani nimeshasikia yote hadi nilipokuja kusimuliwa hicho kisa na aliyenisimulia ni rafiki yangu ambaye aliujua mchezo mzima na alikuwepo kwenye hiyo party ni ndugu wa huyo jamaa! Ila daah siku hizi mapenzi hakuna aisee hata hao wanaume masikini wenyewe nao wana misururu traffic anasubiri acheni tu wanawake waangalie mifuko jamani maana hayo mapenzi ya kweli hayako tena kila mtu msaliti!
 
Back
Top Bottom