Lazima afeli hapo sijui kwanini
My brother alipata mchumba, dada mmoja asili ya ki Asia, nilichoandika hapo mkuu tuliki practice in real life nakupa true story kabisa..
Jamaa ndiye alileta wazo kwa sababu anataka kumuoa huyo binti baada ya mahusiano ya uchumba..
Akanishirikisha nikamwambia haina shida😀 ni wewe tu..
Jamaa akanikabidhi funguo za gari zake 2, akamficha mchumba wake kuhusiana na status halisi aliyokuwa nayo, alimwambia gari ameuza kulipa madeni..
Walikwenda kupanga uswahilini, yule dada alikuwaga amezoea ku drive akaanza kupewa nauli kwenda chuoni, at the time alikuwa mwanafunzi anajiendeleza..
Dada kapambana sana na daladala😁, akirudi maskani ni hadithi za vituko vya kwenye daladala, basi bwana ukapita mwezi, jamaa alikuja kunieleza kwamba imetosha anaona kafaulu tayari, nikamwambia pambana na hali yako, funguo sikupi tumekubaliana miezi mitatu we mwezi mmoja tu unaanza kubadili mawazo, jamaa akanambia anamuonea sana huruma😂..
Mzee wa kushauri nilikuwa nimesimamia msimamo wangu, nikamwambia sasa anza na kumuomba pesa kabisa😂, mwambie upo broke mbaya😂
Jamaa akasafiri kwenda mkoa flani kikazi, huko akawa anampigia mchumba wake simu kwamba hali ni mbaya, hana pesa ya kula, dada anatuma pesa, jamaa anamuuliza umeiotoa wapi? anasema mama alinipatia nikatunza..
Life likasonga, mwezi wa pili, mwezi wa 3, binti alifaulu ule mtihani hata mie sikuamini kabisa😁, niliweka msimamo kwa sababu huyu msichana nishazinguana nae, angefeli ingekuwa fresh tu kwangu.., angefaulu pia ingekua fresh cause bro angekuwa amepata mwanamke sahihi..
Nilimkabidhi jamaa funguo zake akiwa na furaha kinoma, ndoa ilifungwa wiki chache baadae, siku hio nilicheza mziki ukumbini mpaka watu walinishangaa😂..
Na mie nilijipiga siku hio nikawapatia zawadi ya fridge, ngoja niangalie picha kama ipo kipindi natoa zawadi niiweke..
Basi ikawa hivyo, jamaa alinushukuru baadae, wakawa mke na mme..
Mi sio mwandishi mzuri..
Mkuu hii sio hot tea, hii kitu imenitokea na nimei practice kabisa..
Wapo kwenye ndoa miaka michache sasa, wana 2 beautiful daughters na life linasonga..