Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it


giphy.gif
 
Mkuu biashara ya hayo mazao inalipa sana enh? Unaweza nipa mchanganuo wake kama hutojali?

Sent from my SM-A705F using JamiiForums mobile app
Zao la mkonge linalimwa sana Tanga na morogoro, soko lake lipo wala si la kutafuta, kwa Tanga yapo maeneo mengi sana ya kufanyia hicho kilimo, yapo korogwe, hale, pangani, mgombezi na maramba. hayo maeneo yapo karb na viwanda, nikimaanish kazi ya mkulima ni kupanda mbegu tu, na unaanza kuvuna baada ya miaka 4 mpaka mitano, hapo utakuwa huna kazi tena mana wanakuja kkvunia wenyew, production wanfny wenyew kuuza ipo bodi ya wakulima ndo wanapeleka mzigo, ww utakuw unasmamia tu, na uvunaji unakuwa kila baada ya miezi 6.

Tunalima kwa hekta nikimaanisha , heka mbil na nusu....ila kwa makadirio ya kawaida ni kila hekta mill 3 apo umetoa oparation costs .kama mkonge wko uko vzuri..kama una hekta 12, kweny 30 mill unapiga vzuri tu bila shida ukitoa all costs. na hii inakuwa kila baada ya miezi 6. Gharama ya kuupanda haiwez kizidi nusu ukishakatiwa mkonge wako kwa mara ya kwanza. Namaanisha kama umpand hekta 12 unawez ktmia gharam ya mill 13 tu..ila ukivuna unapiga kweny mill 15. Na ukishapanda mkonge ww ni kuvuna tu mana hutopanda tena..utakula ww pamoja na wajukuu zako.

kuna usemi unasema wanaume wa Tanga ni wavivu sana,, ni kweli mana wamewekeza kwenye mkonge, wao ni kutumia pesa tu na kushinda kwenye kahawa na bao. Kuhusu upatikanaji wa mashamba kama utakuwa interested nakutumia fomu ya kuomba shamba ila sna hakika kama deadline itakuwa bado inasoma..

Kama muda wa maombj utakuwa umeisha nitakuelekeza sehem ambayo wanauza mashamba kwa bei rahisi, uende mwenyewe ukafanye negotiation wala ustegemee kwamba nitakuelekeza uende kwa mtu fulani akutaftie shamba mana mm sio dalali, nakuelekeza maeneo ya kupata shamba kwa bei ya kila heka bei isiyozid laki 1.

Ukitaka maelezo zaidi kuna uzi nimeeleza kwa kina sana unaitwa fahamu biashara ya mkonge Mana hapa si maeneo sahihi pa kulieleza hili.

Mimi si mwandishi mzuri ila nahis utakuwa umepata chochote kitu.

Naomba radhi kwa kuingiza mada tofauti wanauzi.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom