Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Mungu anasamehe na kusahau kabisa.

Waraka wa kwanza wa Yohana kwa watu wote.
1:8
Tukisema kwamba hatuna dhambi,twajidanganya wenyewe,Wala kweli haimo mwetu.Tukiziungama dhambi zetu,Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.

Hata mtu akiwa ndani ya Kristo ya kale yote hupita na tazama huwa mapya.

1yohana 2
Yeye asemaye nimemjua Mungu Wala hazishiki amri zake,ni mwongo Wala kweli haipo ndani yake.


Amri kuu ya kwanza ya Mungu iliyojumlisha zote..
"Mpende Bwana Mungu wako kwa Moyo wako wote kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote.

Injili ya Yohana anasema"mkinipenda mtazishika amri zangu'

Pia sehemu nyingine anasema Msidanganyike Mungu hadhihakiwi..chochote apandacho mtu ndicho avunacho.

Kuna watu wamejipangia tu yaani anasema nikifika 50 ndio nitaokoka. Wacha nile dunia.. neema si ipo!
Mungu hadhihakiwi..ukimpenda lazima ufwate maagizo yake.
Kwenye hili tupo wengi tunao jipangia umri fulani tuanze kumtumikia mungu💫☀️🤔😢✨neema yake ituokoe tu.
 
Usiku mwema
FB_IMG_1611763084626.jpg
 
Sawa nimefurah kufahamu hayo,
Ngoja niendelee kujijenga kiroho.
Roho mtakatifu ni mwaminifu Sana.
Anatusaidia kwenye udhaifu wetu maana hatujui kuomba vile itupasavyo

Roman8:26

Hivyohivyo ulivyo anakusaidia maana ndiye msaidizi na kazi yake ni hiyo kwa sababu tu dhaifu na kama tusingekuwa dhaifu basi kusingekuwa na haja ya yeye kuwepo.
Mtumie katika yote.

Ila ana sharti gumu..hakai mahali pachafu
 
Roho mtakatifu ni mwaminifu Sana.
Anatusaidia kwenye udhaifu wetu maana hatujui kuomba vile itupasavyo

Roman8:26

Hivyohivyo ulivyo anakusaidia maana ndiye msaidizi na kazi yake ni hiyo kwa sababu tu dhaifu na kama tusingekuwa dhaifu basi kusingekuwa na haja ya yeye kuwepo.
Mtumie katika yote.

Ila ana sharti gumu..hakai mahali pachafu
Haya mawazo ndo chanzo cha uchafu wa roho zetu.
 
Kwenye hili tupo wengi tunao jipangia umri fulani tuanze kumtumikia munguneema yake ituokoe tu.
Ungakijua saa ambayo mwivu yuaja kuiba,ungelikesha ukimngoja.
Ungelijua saa ambayo utaibiwa ungelikaa ukiwa tayari.


Ni nani aijuaye siku ya kurudi mwana wa Adamu?hata malaika Mbinguni hawajui.

Kuna tenzi moja inaitwa liko lango moja wazi...ubeti wamwisho(4)
Hima ndugu tuingie lango halijafungwa
Likifungwa Mara moja halitafunguliwa"


Pia ukipata muda soma habari za Batimayo na tajiri.

Ukipata muda soma pia mpanzi (The parable)
 
Back
Top Bottom