Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

1584108711084.jpg
 
Bora umeongea na wewe. Natamani kama wale watu walionipa zile sifa wapite hapa waone sijui niwaite.

Saint Anne unakumbuka kwenye ule uzi wa sijui mtag mtu kisha weka sifa yake moja kuna mtu alisema Zoë namuona mbishi hasa kwenye masuala ya kutetea wanawake anaweza akabishana na JF nzima. Akaja mtu akadakia kuwa eti mimi ni mbishi hadi in real life daah.
 
Yawezekana ukiwa haupo nyumbani unakuwa mkorofi.

Mimi siwezi kuwa mkorofi! Naogopa sana watu na hata mtu akinipiga huwa naogopa kumrudishia hata kama nina uwezo huo!

Kuna roommate wangu mmoja alikuwa anapenda sana kunionea kila akinikuta room lazima anizabue bao basi tu kunichokoza! Halafu akawa anasema eti anafanya vile sababu anajua mimi siwezi kumrudishia na kweli sikuwahi kumrudishia maana mtu mwenyewe ukimuangalia hata mkononi hajai basi tu ni vile alinikuta mimi mpole!
 
Mwacheni mwanangu, halafu sijui kapotelea wapi!! Ngoja nimsake.

alikuwepo kule kwenye uzi wa iphone anatafuta brand nzuri ya simu ya kununua kasema eti ameichoka brand ya samsung, mnunulie tu tecno sasa.
 
Mimi siwezi kuwa mkorofi! Naogopa sana watu na hata mtu akinipiga huwa naogopa kumrudishia hata kama nina uwezo huo!

Kuna roommate wangu mmoja alikuwa anapenda sana kunionea kila akinikuta room lazima anizabue bao basi tu kunichokoza! Halafu akawa anasema eti anafanya vile sababu anajua mimi siwezi kumrudishia na kweli sikuwahi kumrudishia maana mtu mwenyewe ukimuangalia hata mkononi hajai basi tu ni vile alinikuta mimi mpole!
Kweli wewe mpole dear hukuwahi hata kumuambia kuwa asiendelee kufanya hivyo
 
Kweli wewe mpole dear hukuwahi hata kumuambia kuwa asiendelee kufanya hivyo

Nilikuwa namuambia ila hilo ndiyo lilikuwa jibu lake kuwa anafanya vile sababu anajua mie siwezi kumrudishia hivyo hawezi kuacha. Kwahiyo ilibidi nikubali tu kuwa punching bag yake.

The good thing ni kwamba alikuwa hanichukii bali alikuwa anafanya vile for fun tu. Hivyo sikuwahi itafsiri kama chuki basi tu nikajikuta nimezoea infact wengine tulishazoea kuonewa bila sababu.
 
Ooh okay , I feel you
Mimi nilikuwaga mpole mno badaae yakanishinda Kila mtu akawa ana take advantage of the situation nikajiapisha hamna atakayekuja kunionea tena ,Naongea siku hizi mno sio mpole tena
 
Sasa wewe kidogo ni kama mimi. Mimi mwenyewe maisha yangu yote ya shule nilikuwaga mpole yaani kiasi kwamba mtu anaweza akaninyang’anya mali yangu badala niichukue nabaki nalia na kusema kwa mwalimu napo nilikuwa naogopa.

Ila nilipofika chuo nikasema sasa basi acha na mimi nianze kuwa muongeaji niache huu ujinga. Ila cha ajabu uongeaji wenyewe eti umekuwa ni wa maandishi nyuma ya keyboard tu ila kuchambana au kubishana na mtu hivi live siwezi.

Nakumbuka kuna dada mmoja chuoni tuliwahi gombana kwenye group la darasani hadi akaleft group nikaona haitoshi nikamfuata inbox nikamchamba hadi akaniblock. Siku hiyo akaniona darasani akasema “enheee afadhali leo nimekuona haya ongea hapa yale yote uliyokuwa unaongea siku ile kwenye group” aisee alinichamba mbona nilinywea nilikuwa mdogo kama piriton ikabidi tu nimuombe msamaha yaishe.

So pamoja na kwamba nimekuwa muongeaji kwa kiasi chake ila bado nina uoga na aibu fulani hivi kwa watu. Nina confidence kwenye uandishi tu ila eti uniite uniambie ongea yale yote uliyokuwa unaandika hata kama ni mazuri nashindwa.
 
Back
Top Bottom