Sasa wewe kidogo ni kama mimi. Mimi mwenyewe maisha yangu yote ya shule nilikuwaga mpole yaani kiasi kwamba mtu anaweza akaninyang’anya mali yangu badala niichukue nabaki nalia na kusema kwa mwalimu napo nilikuwa naogopa.
Ila nilipofika chuo nikasema sasa basi acha na mimi nianze kuwa muongeaji niache huu ujinga. Ila cha ajabu uongeaji wenyewe eti umekuwa ni wa maandishi nyuma ya keyboard tu ila kuchambana au kubishana na mtu hivi live siwezi.
Nakumbuka kuna dada mmoja chuoni tuliwahi gombana kwenye group la darasani hadi akaleft group nikaona haitoshi nikamfuata inbox nikamchamba hadi akaniblock. Siku hiyo akaniona darasani akasema “enheee afadhali leo nimekuona haya ongea hapa yale yote uliyokuwa unaongea siku ile kwenye group” aisee alinichamba mbona nilinywea nilikuwa mdogo kama piriton ikabidi tu nimuombe msamaha yaishe.
So pamoja na kwamba nimekuwa muongeaji kwa kiasi chake ila bado nina uoga na aibu fulani hivi kwa watu. Nina confidence kwenye uandishi tu ila eti uniite uniambie ongea yale yote uliyokuwa unaandika hata kama ni mazuri nashindwa.