Unajua kuna kitabu kimoja nilikuwa nasoma kinaelezea kwa nini ulimwengu upo, na kwa nini umeweza kutokea.
Kinaitwa "Why Does The World Exist: An Existential Detective Story".
Wanakwambia, ulimwengu unaweza ku exist kwa sababu ya imbalance fulani zilizotokea katika nothingness.
Yani, kulikuwa na perfect nothingness, yani tuseme chaji negative na positive zimebalance, kwa hiyo net result ikawa zero.
Basi ile zero ikapata chafya kidogo tu, ilipopiga chafya ikaharibu balance, ikawa kama chafya imeenda kusabisha imbalance, ile imbalance ndiyo ikazaa ulimwengu.
Kwa hivyo, tukirudi kwenye msemo wako wa "Life ins't fair", tunajikumbusha kwamba, if life was fair, it wouldn't exist.
Kwa sababu ujue mama kuzaa mtoto, halafu mtoto akawa mdogo kwa mama si fair.
Fair world ingetaka mtoto na mama wote wawe na umri mmoja, ingetaka mtu asile mnyama (kula mnya si fair kwa mnyama) ingetaka mtu asile mmea kuuua mmea ili uule si fair kwa mmea). Ingetaka mmea usichukue madini ardhini (kuyatoa madini ardhini na kuyaweka kwenye mmea sio fair kwa madini.
Ukitaka life iwe fair, utajikuta unaua life yote.
Sasa chagua, unfair life ambayo unaweza kupambana, au no life at all, which is fair to all?