True that, ila sasa sisi wanaume ni mende ujue since day one like tokea tunazaliwa...kila jalala tumo...lakini kwenu huwa inakuwa special
Nakumbuka nikiwa primary kuna kadada kazuri kazuri kenyewe kumbe kalikuwa kananikubali bila miminkujua, lkn rafikize walikuwa wanajua...
Sasa siku ndio tumeua std 7, that day tulipikiwa wali mchafu na soda za chupa, kale karembo kakaanza kunisaka.Kila nikipita kona hii, naambiwa fulani anakutafuta hahaha.
Basi ile kafanikiwa kuniona, she ran after me, na kunihug like how em girls do in movies.
Nikapewa vizawadi pale, mostly misosi misosi...yaani hapo nipo nashangaa shangaa tu, nilikuwa mpole sana na very shy, mtu wa kitabu sana. Kwanza hapo nawaza nitapata ngapi out of 150 ili niende shule kali.
So i never reacted the way she would expect, tukala kala pale, jamaa zangu wakatokea tukaondoka zetu maana tulikuwa tunakaa mbali na tulipoenda fanyia paper, enzi hizo kama unasoma shule A, std 7 mnapangiwa kwenda kufanya huko shule P kuepuka paper kuvuja.
Since then sikuwahi jua yupo wapi, until some few years back, kashaolewa na ako na watoto na ako anaishi +44