Leo nimetoka posta nimepanda na kaka mmoja kwenye mwendokasi
Huwa nasimama kwenye maungio yale,
Yeye kapandia Jiji.
Kaja kusimama mbele yangu tukawa tunaangaliana..nilikuwa nimeinama alipopanda akanigonga nikashtuka,nikamuangalia nikakuta HB hatari.
Mzuri jamani,amevaa vizuri suti yake,halafu ananukia.
Mwee safari nimeiona fupi,
Naye kasimama palepale hadi mwisho,
Hajasogea hata mbele yake.
Tumeishia kugongana gari ikiyumba..
Mara ahamishie mkono niliposhikilia,
Na mimi hata sikuutoa.
Ila kumuangalia nilikuwa siwezi,nikawa naibia,,nimevaa cap.
Nikasema hapa lazima nimshinde shetani,,wakati wa kushuka ntashuka haraka yasije Kutokea mengine.
Naye kumbe akawa anashukia Mbezi stand.
Aisee gari imesimama,nachukua begi langu pale chini nilikuwa nimeweka
Kaka amesimama tu ananiangalia.
Nilivyomuangalia akageuka kuangalia mlango wa Kutokea.
Nimeishia kutabasamu tu na kuondoka .
Nimeokoka nampenda Yesu.
Wanaume jitahidi muwe mnanukia jamani,
Wakati wa kwenda nilipanda nikakaa mwisho kabisa na wakaka wote,
Aliyekaa pembeni yangu ananuka jasho jamani chaa
Angalau safari yangu ya kurudi imekuwa mubashara.