Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

20230109_162903.jpg
 
Nimeipenda hii:

Huko nyuma katika siku ambazo Ujerumani iligawanywa, ukuta mkubwa ulitenganisha Berlin ya Mashariki na Magharibi.

Siku moja, baadhi ya watu katika Berlin Mashariki walichukua shehena ya lori la taka na kuzitupa upande wa Berlin Magharibi.

Watu wa Berlin Magharibi wangeweza kufanya jambo lile lile, lakini hawakufanya. Badala yake walichukua shehena ya lori la bidhaa za makopo, mkate, maziwa na vyakula vingine, na kuvipanga vizuri upande wa Berlin Mashariki. Na juu ya safu hii waliweka bango hili

“KILA MMOJA HUTOA ALICHO NACHO”

Huh ni ukweli mtupu! Unaweza tu kutoa kile ulichonacho.Una nini ndani yako?

Ni chuki au upendo?
Jeuri au amani?
Kifo au uzima?
uwezo wa kujenga au uwezo wa kuharibu?
Umepata nini kwa miaka mingi?

"KILA MMOJA HUTOA ALICHONACHO"

Fikiria juu yako!

Kuwa na siku njema!
Nice one
 
Back
Top Bottom