Siwezi kudai.
Kuna mmoja alikuja kukopa ya kupeleka vicoba huko.
Akasema akishapeleka ni zamu yake kuchukua.
Nikampa..
Hakunilipa.
Baadaye muda umepita akawa ameumia mguu alidondoka akajigonga goti...Alikuja nyumbani kuomba spirit.
Nikagawia..Nikamuelekeza dawa ya kukausha kidonda haraka anunue.
Akasema hana hela,Nikampa hela ya dawa na nikamwambia ile hela niliyokukopea nimekusamehe.
Kesho yake akaja...anasema ana shida ya hela anunue mahitaji anafanya biashara ya chips.Akiizungusha atanirudishia.
Akataka kiasi,Nikampa ila nilimpa pungufu ya ile aliyotaka...ilipungua kama elfu 10 hivi.
Nimamwambia ungeniambia mapema ningejitahidi kubana matumizi..Jana ndio nilitoa hela ya matumizi yangu na hiyo ndiyo iliyobaki.
Akaondoka.
Jioni akanitafuta,anauliza kama sijaenda tena benki ili nimtolee elfu 10 iliyobaki eti hajanunua tomato na chill sauce!
Nikamwambia sijaenda.
Kesho yake tena akanitafuta..tena akaja nyumbani kabisa...nikamkaribisha nashangaa amekaa kimya,Nikamwambia nakusikiliza..Anasema umesahau??Ni kuhusu ile hela iliyobaki.
Binadamu waswahili ni wajinga sana.