Huku Tanzania ukimkopesha mtu hela unapoteza hela yako na unampoteza na yeye.
Kuna mwingine alikuwa mpendwa mwenzangu..tena kiongozi Fellowship.
Tulipoanza semester nilienda na nguo za mtumba..Mzee wangu alinipa mtaji..nikajumua mtoto wa watu.
Kufika chuo nikamwambia nauza nguo...akaniambia lete nikuuzie maana yeye watu wengi sana wanaenda rum kwake na anajichanganya sana na watu.
Nikampa...alinambia watu wananunua..nikafurahi nikamwambia basi zikiisha utaniambia.
Sikupata hela hata sh mia wala nguo.
Na hakuwahi kuzungumzia chochote na mimi nilikaa kimya hadi leo na nilishasamehe.