Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,566
Salaam Wadau,
Kama umewahi kufika Ubungo, Morocco na Mbezi Louis utakutana na kivuko cha watembea kwa miguu kinachopita juu ya barabara. Japokuwa sehemu hizo zilikuwa na nia ya kurahisisha uvukaji kwa Watembea kwa miguu, lakini namna vilivyotengenezwa vimekuwa kama adhabu kwa wavukaji wake.
Sehemu hizo za kuvuka zimekuwa na mzunguko mrefu usio na maana yoyote kwa wavukaji. Utengenezaji wa sehemu hizi haujazingatia ugonjwa na uwezo wa watu kutembea sehemu ndefu.
Baadhi ya watu wanalazimika kushuka kituo kimoja kabla ili kuepuka kupanda sehemu hizo ambazo ni ndefu mno.
Ipo haja ya sehemu nyingine za kuvuka zirahisishwe ili kutowasumbua watu.