Ndoa za wake wengi ni mateso sana kwa watoto/ wake

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,677
12,244
Ndugu zangu nawasalimu Kwa Jina la jamhuri ya Tanganyika. Mimi ni muumini wa dini ya kiislam Ambae Kwa kiasi Fulani naweza kusema Imani yangu imeteteleka kutokana na baadhi ya matendo ya watu wa Imani ambao nilikuwa na waamini sana ila mwisho wa siku wanafanya mambo kinyume na maelekezo ya Dini.

Katika dini zote tunaamlishwa kufanya mema na kukatazwa kufanya mabaya hivyo sipingani na Imani ya mtu wowote hata kama Hana dini kama afanyi mabaya huyo ni mtu wa Mungu.

Kwenye dini yetu ya kiislam Kuna maamrisho mengi sana mema Ikiwemo.

√ Kusaidia Yatima
√ kuwasaidia wazazi
✓ kusaidia wenye huitaji
√ kutoa sadaka
✓ kufuturisha kwa waliofunga mwezi mtukufu.

Hizo ni baadhi. matendo mema ya sisi waislam yamegawanyika kwenye makundi mawili.

1. Faradhi

2. Sunna

Ili swala la kuoa lipo kwenye kundi la kwanza la faradhi. Ila ili ndoa iwe ndoa Kuna misingi ya kuzingatiwa.

Muhtadha wa andiko langu upo kwenye hizi ndoa za wake Zaidi ya mmoja. Ambayo Mimi naiweka kwenye kundi la sunna maana imeandikwa kuwa "muoe wake Hadi wanne kama mna uwezo".

Hivyo usipo oa wake wengi sio dhambi ila kikubwa ni lazima uwe na uwezo.

Ndoa za wake wengi Kwa nchi yetu changa kiimani, changa kimaendeleo na changa ki uelewa HAZIFAI.

Wenzetu WAarabu wanaouweza wa kuoa Zaidi ya wake mpaka wa 4 kwasababu wanao uwezo kipesa na dini imeanzia Kwao hivyo wanauelewa mpana sana wa Hilo swala.

Watanzania wengi vipato vyetu ni vya kawaida sana hivyo kuoa wake wengi ni sawa na kuipa familia UMASIKINI wa kujitakia.

Kwenye andiko langu hili

Najuta kumtia umasikini Mama yangu

Wachangiaji wengi walinilalamikia kuwa kwanini andiko lote hakuna sehemu nimemtaja baba😭🙆😭🙆

Mimi nimelelewa na wazazi wote wawili baba na mama na Nina mshukuru Mungu sana wazazi wangu wote Bado wapo hai na wanaishi pamoja.

Kitu kilichopelekea nisimgusie mzazi wangu wa kiume kwenye andiko langu la awali ni ile hali ya yeye kuwa na wanawake wengi. Najua nakosea Kwa Mila zetu kuzungumza hivi ila mtanisamehe sizungumzi Kwa Nia mbaya.

Kwa uwezo wa kiTanzania kuanzia cheo cha mkuu wa mkoa kushuka chini awana uwezo wa kumudu kuhudumia wanawake Zaidi ya mmoja.

Hizi ndoa zinaleta mateso makubwa sana Kwa watoto na Huwa zinaleta matabaka sana. Kuna familia Moja kati ya hizo itajaaliwa. Harafu itaona kama inapendelewa.

Kuishi bila kupendelea haiwezekani hivyo Kuna mke atapendelewa yeye na watoto Wake. Hapo ndipo balaa litapoanza kujitokeza.

Baba yangu Kwa nafasi aliyokuwa nayo alikuwa na uwezo wa kuhakikisha watoto Wake wote wanasoma na kupata kazi endapo angekuwa na familia Moja.

Ila Hilo ameshindwa kulifanya kwasababu ya kuhusudu ndoa za wake wengi kitu kilichopelekea baadhi ya watoto kutelekezwa. 😭😭😭

Waliosema ndugu zako wa kweli ni watoto wako wa kuwazaa hawakukosea ila sio watoto wawe wengi kupita kiasi.

Kibinaadam ukiwa na watoto 3 au 4 hivi wanatosha sana. Sasa unakuta mfanyakazi analipwa milioni 1. Ana wake Zaidi ya 4 ana watoto 16. Huku ndugu zake dada, kaka na wadogo zake wote wanamtegemea mtu kama huyu anaweza kweli kuwasaidia watoto Wake.

Ifike kipindi serikali itoe tamko baadhi ya maandiko ya Dini yazingatiwe yasifuatwe kwani yanadhalisha kizazi chenye chuki na visasi na kulirudisha Taifa nyuma😭😭😭

NAPINGA NDOA ZA WAKE WENGI.​
 
Ni wachache saanaaa!!!! 9/1
Sidhani kama wapo na kama wapo upendo wao Huwa wakinafki baraaa hujitokeza baada ya baba Yao kufa ndio utajuta hujui. Kila mtu ataanza kuionyesha sasa rangi yake harisi... 😭😭😭​
 
Kama huna uwezo wa kumpa good life mwanao ni bora usizae.

Binafsi sipendi na sitamani kuzalisha kizazi masikini.
Na sio ndoa za wake wengi tu hata ile kua na watoto wengi au watoto wachache kwa mama tofauti tofauti.

Utafurahia kipindi unawajaza mimba pisi kali, majukumu yakianza unazeeka kabla ya muda.
 
Kama huna uwezo wa kumpa good life mwanao ni bora usizae.

Binafsi sipendi na sitamani kuzalisha kizazi masikini.
Na sio ndoa za wake wengi tu hata ile kua na watoto wengi au watoto wachache kwa mama tofauti tofauti.

Utafurahia kipindi unawajaza mimba pisi kali, majukumu yakianza unazeeka kabla ya muda.
Bravo sana . Hicho ndio nilicho kuwa namaanisha. Ni kweli Bora usiwe na mtoto kabisa
 
Kwanza Nina Shaka na uislamu wako!

Lakini sishangai Kama ulivyo sema umetetereka kiimani bado kutangaza tu umekufuru dini.

Majibu kwa hoja zako kuu.

1.ndoa za mitala hazifai kwa sababu za kiuchumi!.

Dini imesema uoe ukiwa na uwezo sio uoe tu Kisha watu wateseke na uwezo Ni khaswa kiuchumi na kiafya(nguvu za kiume),manake kiuchumi kulingana na Sheria ya dini Ni uweke usawa mke mmoja ukimnunulia gari bc na mwengine lazima umnunulie tofaut na hvyo unapata dhambi Mana inakuwa haufanyi uadilifu ,vivyo hvyo katika kula,mavazi n.k

💥Hvy usilaumu dini kuweke hii Sheria Mana lengo Ni kuepusha zinaa Mana mwanaume Ni MTU wa matamatio Sanaa, mlaumu baba yako kwa kutofuata Sheria kikamilifu manake hakukidhi vgezo vya kuoa wake wengi.
2.Ndoa za mitala hazifai kweny nchi zetu.

Huo Ni uongo mkubwa unataka uniambie hzi nchi watu wenye Ela hamna ama ni vipi?

Na katika dini uwezo unaangaliwa katika mahtaj muhmu ya kibinadamu malazi,malazi, chakula n.k, uwezo c kumiliki mabilioni.

💠Wew unapinga ndoa hzo kwa chuki bnafc hyo Sheria imewekwa kwasababu Kama hz:

1.mwanaume kukaa na mke mmoja Ni ngumu lazma atmchoka kihisia c kimapenzi hvy atatamani nje ,so dini imemkataza znaa manake atateseka ndo mana akafanyiwa wepec kwa kuoa Zaid ya mke mmoja.

2.wanawake Ni wengi kuliko wanaume SKU zote Kuna wengne Ni wajane,wametelekezwa inategemea Nani awao?(lengo kubwa la dini Ni kupinga znaa).

ACHA CHUKI NA DINI ZA WATU ,MLAUMU BABA YAKO KWA KUTOKIDHI VIGEZO VYA KUOA WAKE WENGI
 
Back
Top Bottom