SAUT siyo Chuo salama kwa Wanafunzi

SAUT siyo Chuo salama kwa Wanafunzi

Ukiwa Msabato wanakuwekea test jumamosi makusudi kabisa
Mbona Waislam wanafanya test Ijumaa na hawalalamiki? Shida hukusoma prospectus kabla ya kujiunga na chuo. Hayo mambo yote yameelezwa kule. Ilitakuwa uwe na taarifa sahihi kuakikisha kanuni za chuo zinaendana na imani yako kabla ya kujiunga na chuo.
 
Ushauri kwa Kaka, Dada, Mama, Baba, Mjomba, Shangazi na walezi usije mshauri kijana wako wa kike au wa kiume kuomba chuo Cha SAUT-Malimbe Mwanza tegemea yafuatayo

* Carry ya kutafutiwa na mhadhiri ushaidi waulize wanafunzi wa BAMC-3 juu ya course ya TV production

* Incomplete kwenye matokeo ni jambo la kawaida unaweza pata incomplete ukiwa first year mpaka unafika third year unayo licha ya juhudi binafsi kuiondoa kwenye hili wanafunzi wa PR ni wahanga na mashaidi wazuri Kama una ndugu anasoma uliza.

* Dharau wafanyakazi wengi SAUT sio wawajibikaji kutimiza wajibu wao huona Kama ni hisani pia dharau kwa wanafunzi mfano ni ofisi ya IT

* Wanafunzi kurudia course pale suala la incomplete likiwa ngumu mwanafunzi hushauri kurudia course ( carry) na kulipia kiasi Cha 50,000/=Tsh wakati sio kosa lake ni kosa la mfumo SIM

* Penalty ukiwa na deni la chuo na muda ukipita wa kulipa ndugu yangu penalty inakuhusu 100,000/= hata Kama una daiwa 10,000/=

* Kukosa ID ya kufanyia mtihani ada umelipa huna deni lakini kukosa ID ya kufanya mtihani ni kawaida hili ndio tatizo kubwa kwa Sasa mpaka muda huu watu hawajui hiyo jumatatu wataingia kwenye chumba Cha mtihani au laa.

* Chuo kujiendesha kienyeji. Yaani unawakusanya wanafunzi wa course zote katika chumba kimoja halafu wanasimama watu mbele wanaita majina ya ID za mitihani [emoji15][emoji15]

Haya nikwa machache tu uzuri humu wadau wapo wengi Sana watakuja kuongezea.

"Zingatia ushauri huu utakuja kunishukuru baadaye"
Mkuu, umeshasoma vyuo vingapi hapa nchini?
 
Saut ndani ya shutuma nzito za kuzaa bila kutumia uzazi wa mpango
 
Dr.FatherApolinary Ndasi si ndiyo mkuu wenu?
Kwanini msimfuate mumueleze?
Ni mtu makini sana yule.
 
Naona unatumika kijana kuchafua chuo Saut ni moja ya vyuo bora sana wewe ndio tatizo ongeza msuli hpo msuli wake mkubwa hakuna kubebana
 
Tatizo la SAUT sio chuo au wahadhiri, ila ni wanafunzi. Take that from me. Wanafunzi wanapenda mtelemko, wanataka kubebwa kuliko vyuo vingine. Sasa wanapo shindwa kubebwa huanza lawama.
Uko sahihi mkuu wamezoea kubebwa hawataki kusoma wanataka kucheza alafu wapewe degree za burebure
 
Mkuu hujapunguza kitu kabisa. Mdogo wangu kamaliza Diploma hapo mwaka jana hayo mambo kayakuta.

Kuna jambo hujagusa, SAUT ndio chuo kinaongoza Tanzania kwa wanafunzi kujifungua hasa ukienda BaEd huwa wanataniwa kwamba wanazaa wanafunzi wao wenyewe. Hili sijabahatisha kulisema, nimezungukavyuo vingi kwenye matembezi yangu na nina marafiki wengi ila SAUT kwa kulea watoto ni next level
Hiyo ya kuzaa ni karubia vyuo vyote ambavyo vina kozi za ualimu,sijajua kwanini.
 
Nilishasema mimi Tanzania vyuo ni vitatu tu
Ardhi University kama unataka kuwa mbobevu wa ukandarasi wa majengo na usanifu ramani na mambo ya ardhi.

SUA kama unataka kuwa mbobevu wa mambo ya kilimo

MZUMBE kama unataka uwe mbobevu wa maswala ya sheria uongozi na utawala bora

Vingine ni takataka tu
Walau St. Joseph i think
 
Naona unatumika kijana kuchafua chuo Saut ni moja ya vyuo bora sana wewe ndio tatizo ongeza msuli hpo msuli wake mkubwa hakuna kubebana
Nani anitumie mkuu ukweli lazima usemwe mfano muda huu wanafunzi walio kosa ID wamekusanywa M 11 mtindo ni ule ule Kama mwalimu wa Shule ya msingi anagawa mitihani
 
Nilikua nataka niwashauri ndugu Zangu Wajiunge. Lakini Baada ya Kupitia Huu Uzi. Nimegundua SAUT ni miyeyusho.
 
Mnakaa tu kusifia ujinga eti vyuo Bora sijui ni udsm, sijui wapi haya tuambieni hivyo Bora vimeleta mchango gani katika kuitoa Tanzania katika umasikini uliokithiri?

Mbona kama nchi ikitaka kufanya kazi za kitaalamu esp, katika field za engineering, medicine, IT lazima waemploy experts kutoka nje ya nchi, kwa nini wasichukue hao waliotoka vyuo Bora? Upuuzi tu mavyuo yote Tanzania ni Yale Yale

Bora hata SAUT Kuna pisi za kueleweka[emoji16], ila ni kweli hiki chuo kijirekebishe kidogo wamejisahau mno, hasa pale IT Kuna uozo.
Chuo kikuu ni chuo kikuu tu shida wengi wanaamini chuo kuwa na magorofa ndo chuo kikuu
 
Wewe ni mwanafunzi mpuuzi sana...nawashauri walimu wenu wawakamate haswa ikibidi mdisco kabisa vilaza nyie...
Hamtaki kusoma alafu mnataka kufaulu?...mmechanganyikiwa kweli...
Enzi zangu wakati nafundisha chuo mtu kama wewe lazima nikutoe nishai...sipendi watu vilaza...
Kma ww ulikuwa lecture basi ni mjinga sana tena sana
 
Kma ww ulikuwa lecture basi ni mjinga sana tena sana
Hawa wote Wana subili ID za paper muda huu wanao tetea udhaifu wa SAUT Wana shida
IMG_20220701_105112_899.jpg
 
Back
Top Bottom