Mlimamrefu
Member
- Aug 1, 2021
- 27
- 93
Kwa mashtaka yaliyosomwa leo tarehe 23 Agosti 2021 ni wazi serikali imejipanga ipasavyo kwa kesi hii ya Mbowe ya ugaidi.
Serikali kuwa mashahidi 24 na vielelezo 19 siyo mchezo. Sasa tunafahamu kwa nini IGP alilizungumzia hii kesi kwa kujiamini sana na kueleza kuwa Mbowe kama ni mkristo mkweli atawaeleza ukweli wafuasi wake. Yote kwa yote, mahakama ndicho chombo cha juu cha kutoa hukumu.
Kupitia hukumu hiyo tutajua ukweli wa jambo hili. Kwa hatua iliyofikia kesi hii, ni vyema sasa tuiache mahakama ifanye kazi yake. Mabango na kauli za kisiasa kutoka Chadema sasa siyo mahali pake. Bahati nzuri katiba za vyama vyote vya siasa vinasisitiza juu ya kutambua utawala wa kisheria ambapo masuala ya mahakamani yanaachwa kwa mahakama kuamua na siyo kuyaleta kwenye majukwaa ya kisiasa.
Tutaishangaza dunia ikiwa bado chama fulani kitaendelea na kuweka mashinikizo nje ya mahakama. Pamoja na kwamba shinikizo zenyewe hazina hata nguvu ya kufungua soda na haziwezi kubadili lolote kuhusu mwenendo wa hii kesi, bado ni bora tukaachana na kuonesha shinikizo hizo ambazo kwangu naziona ni za kitoto na zinazidi tu kuwadhalilisha wanaoziweka.
Court decisions are based on what the law says and what the evidence proves. There is no place in the courts for suspicion, bias or favouritism. Tuachane na hizo empty rhetoric