Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,106
Leo tumeona Polisi wamedai kumkamata mmiliki wa akaunti ya X inayotambulika kwa JINA la Sukunuku; mara tu polisi walipotaka hayo mawakili binafsi wengi wameonyesha nia ya kusimamia kesi hiyo huku baadhi wakiweka wazi kwamba watashinda kesi husika mapema kabisa.
Mmoja wa mawakili ndugu Madeleka ameeleza ugumu wa kesi ya mtandao kwamba ili uthibitishe upotoshaji lazima uonyeshe ukweli jambo ambalo kwenye kesi ambazo uandaliwa kwa hisia za mpelelezi nivigumu kupata ushahidi wa kuishawishi mahakama.
Upande mwingine wanaharakati wanaeleza kwamba pamoja na sheria ya cyber kuwepo ni vigumu kuthibitisha makosa yaliyoainishwa katika sheria hiyo na hivyo kushindwa kesi kwa Jamuhuri ni jambo la kawaida.
Wapo wengine wanaodai kwamba sheria hii ni ngumu kutekelezeka hasa ikizingatiwa kwamba mwana CCM akitoa lugha fulani hazitafsiriwi na jeshi la polisi kama matusi. Mfano anatajwa Nape Nauye kwamba mara kadhaa ametukana mtandaoni lakini hakuna aliyewahi kumkamata. Viongozi waandamizi wa serikali pia utukana lakini hakuna aliyewahi kukamatwa jambo linaloleta tafsiri kwamba sheria hizi zimeundwa kwaajili ya wapinzani na siyo watu wote.
kulingana na mitizamo hii naamini imewafanya mawakili wengi kuona wanaokamatwa wanaonewa na hivyo kujitolea kuwasimamia lakini pia jeshi la Polisi limekuwa halichukulii serious kesi hizi hasa wakitambua kwamba hawatendi haki kwa watu wote bali wanakandamiza kundi flani
Kwa upande wangu naamini hali hii imepelekea wavunjaji wa sheria kuwa na watetezi wengi hasa sheria zinazolinda maslahi ya wanasiasa watawala. Hakuna mwananchi anayechukizwa na watoe matusi kwa sababu wameona watoa matusi nao wana hoja isipokuwa katika kuwasilisha malalamiko yao wanaweka na maeneo ya udhalilishaji na yanayotweza utu.
Way foward: Tukamate kwanza watawala na kuwafungia ili walio nje ya utawala wajifunze. Nazungumza haya nikikumbuka alivyofanyiwa NONDO wa ACT......akahesabika kama gaidi leo anakula meza moja na watawala