ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,054
- 49,737
Serikali imesema italipa Bilioni 260 Kwa Kampuni ya Indiana Resources kama itashindwa kwenye kesi waliyofungua kupinga hukumu ya awali.
Cha kushangaza Wakili Mkuu wa Serikali anasema kabisa kwamba kama tutashindwa, lazima tulipe na ameji commit Kwa maandishi kabisa.
Viongozi wa awamu ya 5 wameitia hasara sana Nchi hii Kwa maamuzi ya kukurupuka wakati wangeweza kujadiliana na hao wawekezaji waone jinsi ya kutatua badala ya kutumia Nguvu ambazo mwisho wa siku zinaahirisha tatizo badala ya kutatua na kuleta hasara kubwa Kwa Wananchi.
Mambo kama haya yanakera na kutia hasira sana.
My Take
Inasikitisha sana jinsi haya mapesa yanavyoliwa Kwa huu ujambazi wa kalamu.
Pamoja ya kwamba ni kesi ila inatakiwa uchunguzi ufanyike kwamba ni nani wananufaika na hii michongo na Dili za wizi wa kutumia kalamu.
=====
Serikali ya Tanzania imeridhia kwa maandishi katika Baraza la Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kulipa fidia ya Dola milioni 109 za Marekani (Sh260 bilioni) kwa kampuni ya Indiana Resources endapo itashindwa maombi ya kupinga malipo hayo.
Serikali inaomba kubatilishwa utekelezaji wa hukumu chini ya kifungu cha 50(2)(a) na (b) cha Mkataba wa ICSID ikiwasilisha hoja 15, ikipendekeza kufuta hukumu ya kulipa fidia ya kiasi hicho cha fedha.
Hukumu iliyotolewa na ICSID Julai 14, mwaka huu iliitaka Serikali ya Tanzania kulipa kiasi hicho cha fedha kwa kampuni ya madini ya Indiana Resources iliyokuwa ikimiliki leseni ya kuhodhi ardhi katika eneo la Mradi wa Nikeli wa Ntaka Hill, uliokuwa Wilaya ya Nachingwea.
Akizungumzia suala hilo, Wakili Mkuu wa Serikali, Dk Boniphace Luhende ameiambia Mwananchi Digital kuwa;
“Ukweli ni kwamba, Serikali imewasilisha maombi ya kupinga. Hii ni nafasi ya mwisho kwa Serikali kuipinga, endapo itashindwa itabidi kulipa kama ilivyoamriwa.”
Chanzo: Mwananchi