Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,036
- 20,338
Kitatumika kuimbishia watoto.Naona tayari michakato ya sheria iko jikoni mahakama kuanza kutumia Kiswahili mwanzo mwisho tofauti na sasa ambapo dokomenti zote huwa za kiingereza sasa baada ya sheria hii hakimu au mwanasheria yeyote itamlazimu atumie lugha ya kiswahili ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande wa BOT nao pia sheria iko jikoni hatua za mwisho mwisho zimefika kuwa mikataba yote ya kifedha itafanyika kwa lugha hadhim ya Kiswahili. Hii inamaana kuwa hadi risiti za mashine hazitakuwa za kizungu bali kwa lugha ya Kiswahili, haya ni pamoja na Pro foma, Delivari note, bili of ladingi na dokomenti zote unazozijuwa wewe ikiwamo za benki zitalazimika kutumia lugha ya Kiswahili.
Swali la msingi je hizi shule za inglishi midia zitakuwa na kazi gani au wataenda kukitumia kiingereza chao huko Uganda na Zambia.
Na kwanini serikali isipige jiwe katikati na kutunga sheria kuwa kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu lugha ya kufundishia iwe Kiswahili na lugha zingine kama Kiingereza na lugha zingine za kigeni ziwe kama masomo.
Hii italeta maana zaidi kuliko hivi sasa taifa lina dobo standadi kwani wengine wanasoma kwa kizungu na wengine kwa Kiswahili hii haileti usawa hata kidogo.
Mbona mataifa mengi nje ya bara la Afrika yanatumia lugha zao kama Korea Kaskazini, Uchina, Urusi, Cuba na mataifa mengi madogo madogo yanatumia lugha zao kama Falme za kiarabu nyingi wanatumia Kiarabu kwani lugha ya mababu zao. Kwanini sisi bara kubwa kuzidi yote duniani hata kanchi kamoja kasiwepo ka kutumia lugha yake, ukiangalia kuna wakati inatia hadi aibu kuona nchi nyingi za kiafrika zinatumia hadi kiingereza na kifaransa kuimba nyimbo yao ya taifa kanakwamba hilo taifa halina lugha yoyote zaidi ya Kiingereza au kifaransa. Huu ni utumwa mbaya uliopitiliza naamini hata Mungu mwenyewe anachanganyikiwa kwani anaangalia eneo ambalo aliliumba mwenyewe na kuweka watu wake pale na lugha yao baadaye wanamwomba kwa lugha nyingine kwana hawezi kuwa sikiliza.
Naona kuna haja ya kujikomboa kutoka katika utumwa wa kifikra.
Na kanisa ndilo limekuwa mstari wa mbele sana kuhakikisha lugha za asili zinapotea kwani ukija huku kwetu kanisani unaweza kushangaa maana utakuta wote tunajua kiswahili na tunajuana na hakuna mgeni wote ni wandengereko lakini anawekwa mkalimani au mchungaji au nabii au mtume anaongea kizungu utazani yupo ulaya au Amerika, nikama sifa hivi kuwa mzungu.. kwa waislam pia hivyo hivyo yaani mpaka ujilaze katika rahaja za kiarabu ndiyo uonekane sasa safi kwa Mungu.
Mimi pamoja na kulelewa na kusoma kwa sadaka huwa sielewi huyu Mungu wetu wa kikristu na wa waislam kwanini huyu Mungu anashida gani na lugha zetu? kwani hizi lugha zina najisi? maana kanisani bila kizungu ibada haiendi kama zamani bila Kilatini ndani ya kanisa la Roma misa hakuna. Msikitini bila kiarabu tena kile cha kikureshi hakuna ibada hii inamaana gani mbona kama utumwa. Nakama Kiswahili kinanajisi basi hawa watu wa dini waseme tukiache kabisa.
Naipongeza serikali ya awamu ya tano ila msipige pembeni pigeni katikati kieleweke ndiyo maana huwa mnasema huku kwenu ndani ya chama kuwa serikali inapewa Jembe na Nyundo basi kama mmepewa msiwe waoga tumieni hizo zana wengine walishindwa. Sehemu ya kutumia Jembe litumike kama lote na sehemu ya kutumia nyundo itumike sisi watu wa roho tunaelewa hizi mithali.
Nimeshuhudia kwa mara ya kwanza mwalimu wa kiswahili Mkenya akiwa darasani shule ya msingi huko Afrika ya Kusini akifundisha kiswahili na watoto wa kisauzi wakionyesha kufurahia na wakitoa komenti kuwa maneno mengi Kiswahili kimeiba maneno kutoka katika lugha ya Kizulu, Shona, sesoto, Kosa na kiswana huku wakiwa wanasahau kuwa kiswahili ni kibantu.
Hii ni kazi ya awamu ya tano.
Mtoto wa Mchungaji,
Nawasilisha.
Ukiongea kidogo unachanganya "You know"