Tukubali tu Kiingereza sio lugha yetu katika masuala mazito, tusiwe watumwa

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,686
46,373
Nimeangilia kesi kati ya Winshear Gold Corp dhidi ya serikali ya Tanzania huko ICSID. Ukweli usemwe ni aibu tupu kwa upande wa serikali hasa katika lugha, "the the the" ni nyingi sana , sijui kwa nini walikubali kutumia Kingereza katika kesi muhimu kama hii huku ikijulikana wazi Kingereza sio lugha rafiki kabisa kwa Watanzania wengi hata maprofesa.

Ni wakati sasa mikataba yote ya serikali na wawekezaji kuwa katika Kiswahili na pia kesi, usuluhishi na mambo yote ya uwekezaji yafanyike katika Kiswahili. Hao wawekezaji wanaozitaka mali za Tanzania watafute wakalimani wa kuwatafsiria katika lugha zao.

Ni wakati sasa wa kuukubali ukweli na kuachana na utumwa wa lugha.

Mawakili wa serikali katika hiyo kesi wakate rufaa waseme lugha ya Kiingereza ni tatizo kwao kuelewa na kufanya defense.
 
Mimi nafikiri ma CEO wetu kutwa hawapo ofisini wakihudhuria vikao vya rais, vikao vya kuapishwa wenzao, vikao vya CCM, kusafiri baina ya Dodoma na DSM, uteuzi hauzingatii ujuzi wa kina wa mabosi hawa waTanzania wanaokutana na watu wa makampuni ya kimataifa, hawajui jinsi makampuni ya kimataifa yanavyofanya kazi au jinsi inavyopata mitaji n.k

Kutoka maktaba :

Majina ya Prof. Abdulkarim Hamis Mruma na waziri Sospeter M. Muhongo (mbunge) vigogo wa madini Tanzania yaibuka .....

HALI INAVYOKUWA KATIKA TRIBUNAL huko mahakama za nje

22 March 2023
Winshear Gold Corp. v. United Republic of Tanzania (ICSID Case No. ARB/20/25)Hearing Day 3 - Video 1 - 15 February 2023



Source : ICSID


Kwako wewe Professor Abdulkarim Hamis Mruma kutoka GST Tanzania Professor wa Geology unaweza kutuchanganulia appendix / kiambatanisho ili ... pia Director of legal Services Edwin Simon Igenge Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Edwin Igenge unaweza kutufafanulia sheria ya makampuni .....
 
Naona ingetafutwa namna kila mtu apate nafasi ya kujieleza kwa ufasaha kwa lugha yake
Kutokujua lugha haina maana hujui jambo
Hata kesi ikiendeshwa kiluguru hatushindi. Nikuhakikisgie kuwa tatizo letu siyo lugha. Chukulia bunge lako unaloliita tukifu limeuza nchi bila hata kujua kuwa wamepitisha nini.

Hapo hata muambiwe mjitetee kiluguru hamtaweza kushinda. Mkataba umeandikwa kuwa mmekabidhi kila kitu milele. Mkishtakiwa mtasema tukikuwa hatujui?
 
Tanzania nchi ya kipumbavu sana we are not putting ourselves into universal platforms ndio upumbavu hadi Rais ana sign kitu cha kipumbavu
Mimi nafikiri ma CEO wetu kutwa hawapo ofisini wakhudhuria vikao vya rais, vikao vya kuapishwa wenzao, vikao vya CCM, kusafiri baina ya Dodoma na DSM, uteuzi hauzingatii ujuzi wa kina wa mabosi hawa waTanzania wanaokutana na watu wa makampuni ya kimataifa, hawajui jinsi makampuni ya kimataifa yanavyofanya kazi au jinsi inavyopata mitaji n.k
 
Back
Top Bottom