Sasa Kiingereza kitakuwa na kazi gani?

ajabu hao wanaoshadadia kiswahili watoto wao wanawapeleka english medium!

"akili za kuambiwa changanya na zako" by JK
 
Sio kila mtu anaweza hivyo mkuu, mahakama pasikie tu, ukishakuwa mtuhumiwa lazima upate wenge hutaweza think straight, ndio maana wanashauri upate usaidizi,

Hata mawakili wenyewe wanaoshtakiwa wanaweka mawakili.
Ni uoga tu tuliojijengea.
 
Hii inatoka na ukoloni. Mkoloni alitufundisha ili tumtumikie na siyo tuelewe na kujitegeme. Ndiyo kisa unaona watu wanasema eti tukisoma kwa kiswahili tutashindwa kufanya kazi UN, nje ya nchi na kadhalika. Watz US hata 30 elfu hawafiki! Ukiwa na ujuzi wa maana na siyo wa kukariri hata kama hujui lugha fulani mtu atakuajiri tu.
Kweli kabisa mkuu!!!
Kiswahili ni lugha yetu ya Taifa......lazima tuiheshimu na kuitunza.
Hao wakenya Walishakitangaza kiswahili kama lugha yao ya Taifa....hapa kwetu kuna watu wanataka tuongee kiingereza.
 
Mkuu kusema kwamba lugha ikiwa kiswahili mteja ataweza kusimama mwenyewe hiyo ni haiwezekani mkuu. Ipo hivi;

Mahakamani kama mteja yupo na anawakilishwa na wakili huwa tunatumia kiswanglish ni mara chache na mahakama chache hasa kuu na rufaa ndio utakuta kiingereza mwanzo mwisho ila mabaraza ya ardhi wilaya, mahakama ya wilaya hadi hakimu mkazi mara zote lugha za uwasilishi kwa mdomo ni mbili labda zikitokea terminology ndio unakuta wakili anasema kwa kiingereza na mteja atafafanuliwa na ama Mwenyekiti wa baraza au hakimu

Ingekuwa kutumia lugha kunawezesha mtu kujitetea mwenyewe Marekani na Ulaya wasingekuwa na mawakili mahakamani. Tafsiri ya lugha kisheria ni tofauti na lugha ya maongezi.

Sasa yale maneno ya kilatin tutayawekaje kwa kiswahili?

Kuna faida kweli ila faida ni ndogo sana ukilinganisha na hasara. Serikali itakosa mapato na fani ya sheria itadumaa japo lugha itakuwa.

Wateja wataleta ujuaji wataenda mahakamani watapigwa chini mwisho wataanza kusema mahakimu ni wala rushwa kama ilivyo mahakama za mwanzo zinazotumia kiswahili au mabaraza ya kata.
Kutumia kiswahili mahakamani kutasaidia sana kupata haki.
Kuna jamaa alikuwa kaandikiwa barua ya kesi yake kukatiwa rufaa. Barua ipo kwa kiingereza. Akawa ameniletea nimsaidie kutafsiri. Huoni kuwa hilo ni tatizo?
 
Alishinda kwa point za kisheria au kwa technicalities?

Kushinda au kushindwa daawa kuna factors nyingi lakini hilo la mtu kujitetea mwenyewe bila wakili eti tu kwasababu anaweza kufuatilia lugha halipo.

Msamiati wa sheria wenyewe tu ni lugha ndani ya lugha iwe kiingereza au kiswahili.
Njia yoyote itayokupa ushindi ndiyo sahihi mkuu.
 
Kweli kabisa mkuu!!!
Kiswahili ni lugha yetu ya Taifa......lazima tuiheshimu na kuitunza.
Hao wakenya Walishakitangaza kiswahili kama lugha yao ya Taifa....hapa kwetu kuna watu wanataka tuongee kiingereza.
Tena katika nchi za Africa tuna bahati sana. Hakuna nchi inayounganishwa na lugha moja kama sisi hivyo wanaishia kutumia lugha za kigeni. Sisi tumebarikiwa kiswahili badala ya kukitumia tunaiga wengine kama watu wasio na ubongo.
 
Na kwa miaka yote hiyo kiingereza ndiyo lugha ya kufundishia na yashughuli za kiserikali na hakuna chochote cha maana kwa hao wasomi wa kiingereza.
Ni wasomi wa kukariri kwasababu walikuwa hawaelewi walichokuwa wanafundishwa. Ukifika form one wanakwambia kariri tu utaelewa mbele.
 
Tena katika nchi za Africa tuna bahati sana. Hakuna nchi inayounganishwa na lugha moja kama sisi hivyo wanaishia kutumia lugha za kigeni. Sisi tumebarikiwa kiswahili badala ya kukitumia tunaiga wengine kama watu wasio na ubongo.
Huko Cameroon na baadhi ya nchi za magharibi ya Africa wanalumbana na kutengana eti tu kuna wanaoongea Kifaransa na wengine Kiingereza.
Yaani ni tafrani. Sisi ka kiswahili ketu kametufanya hata baada ya muda lafudhi za kikabila zitaondoka kabisa tutabaki na lugha moja ya KISWAHILI tu.
 
ajabu hao wanaoshadadia kiswahili watoto wao wanawapeleka english medium!

"akili za kuambiwa changanya na zako" by JK
Ni asilimia ngapi ya watoto hapa Tz wanasoma hizo english medium ukilinganisha na shule za serikali?.
Usipende kuongeaongea tu mkuu.
 
Tunapo elekea tutapata rais atakaye futa elimu ya darasani endeleeni na huu undezi mtafanikiwa kwa hili mtakuja na madarasa yanini turudi chini ya miti Mabutu Seseseko alifikia kukataa majina ya kuiga haya!! Mdogomdogo Nyerere alisema ukionja nyama ya binadamu mwenzako ni hatari
 
Kutumia kiswahili mahakamani kutasaidia sana kupata haki.
Kuna jamaa alikuwa kaandikiwa barua ya kesi yake kukatiwa rufaa. Barua ipo kwa kiingereza. Akawa ameniletea nimsaidie kutafsiri. Huoni kuwa hilo ni tatizo?

Haki haipatikani kwenye lugha mkuu, kutafsiri sheria sio kutafsiri lugha hivi ni vitu viwili tofauti.

Watanzania watajua tu maneno ya kisheria kwa kiswahili na sio namna yakutumia sheria husika wala kuzitafsiri.
 
Mjumbe akiwepo utapata nini toka kwake?.Nchi hii ina miaka zaidi 59 inatumia kiingereza katika masomo na shughuli za kiserikali,vipi sasa hakuna huyo mjumbe?Vp bado tupo nyuma huko international?.

Ulielewa comment yangu mkuu? Rudi kausome upya utaelewa mantiki yangu kwenye iyo comment
 
Njia yoyote itayokupa ushindi ndiyo sahihi mkuu.

Duuh!

Huo pia ni ukweli usiopingika na asante kwa kunikumbusha mkuu.

Ila mkuu siamini kama kuna lengo la maana la kubadlisha lugha inayotumika mahakamani au kuwa badiliko hilo litaleta tofauti yeyote kwenye kutenda na kupata haki kwa mtu mwenye daawa.
 
Ulielewa comment yangu mkuu? Rudi kausome upya utaelewa mantiki yangu kwenye iyo comment
Mkuu! Ulilijibu swali langu kwa kuonesha kuwa nchi yetu haiwezi kulinganishwa na China kwa sababu China ni sehemu ya nchi zilizoendelea(G12). Lakini ukashwindwa kuhusianisha na mada jadiliwa.Kifupi ulipaswa ujue kuwa China iliweza kufikia uchumi wa juu bila ya kukitumia kiingereza kama lugha ya kufundishia na lugha ya shughuli za kiserikali,bali wao walifundisha na kuongozana kwa lugha yao ya kichina na kuleta mageuzi ya kiuchumi duniani.

Kifupi kiingereza kinazidumaza tu nchi zinazo lazimisha kutumia kiingereza kwa asilimia 90,ili hali kiingereza si lugha asili ya nchi hizo.
 
Sheria ni taaluma hivyo swala la mawakili kuendelea kuhitajika bado liko pale pale.

Mfano uingereza lugha yao ni kingereza sheria zipo kwa kingereza na bado mawakili wanendelea kutumika.
Kuna wajinga wanafikiri wanaweza kwenda mahakamani bila wakili kwa sababu tu wanajua Kiswahili. Duh.
 
Duuh!

Huo pia ni ukweli usiopingika na asante kwa kunikumbusha mkuu.

Ila mkuu siamini kama kuna lengo la maana la kubadlisha lugha inayotumika mahakamani au kuwa badiliko hilo litaleta tofauti yeyote kwenye kutenda na kupata haki kwa mtu mwenye daawa.
Hivi unajua mkuu kuwa hapa Tz kuna takribani asilimia 40 ya watz hawawezi kuongea vizuri hikihiki kiswahili chetu?
Na unajua kuwa takribani asilimia 70 ya watz wa kawaida(wasiojua kiingereza) ndiyo washitakiwa wengi hapa Tz?.
Na unajua kuwa ni sehemu ya haki ya mshtakiwa kujua kwa asilimia 90 mwenendo wa kesi yake ikiwa ni pamoja na kuielewa lugha inayoendeshewa kesi?.
Mkuu!Nadhani kiingereza mahakamani kimepelekea watu wengi sana kuhukumia kionezi.
 
Back
Top Bottom