Sarafina - Mtunzi Nyemo Chilongani

Sarafina - Mtunzi Nyemo Chilongani

SEHEMU YA 121...

“Haijalishi mke wangu, hata ukipita mwaka mzima, jua kuna siku mtoto wetu atakuwa mikononi mwetu,” alisema Richard, japokuwa alikuwa akizungumza kwa kujiamini lakini moyo wake haukuwa na imani hata kidogo.

Wakati akizungumza hayo na mkewe mara akasikia simu yake ikianza kuita. Akaitoa mfukoni mwake na kuiangalia. Namba ilikuwa ngeni, alitamani sana kuipokea lakini kwa kipindi hicho haukuwa muda sahihi wa kuipokea simu hiyo kwani alihitaji kuzungumza na mkewe.

Mpigaji hakukata, ilipokatika, akapiga tena na tena mpaka kuwa kero na hivyo Richard kuipokea na kuipeleka sikioni. Akasikia sauti nzito kutoka upande wa pili, alikuwa mwanaume ambaye alijitambulisha kama polisi na kumpa taarifa kwamba kuna mtu alitaka kuonana naye hapo.

“Nani?” aliuliza.
“Kijana mmoja! Amejitambulisha kwamba yeye ni mganga,” alijibu polisi huyo.
“Nimsaidie nini?”
“Kwamba anataka kuonana na wewe ili uweze kumpata mtoto wako,” alisema polisi, moyo wa Richard ukapiga paa.
“Ni mganga!”
“Ndiyo!”
“Sasa mimi na waganga wapi na wapi?”
“Naomba uje kumsikiliza!”
“Sawa nakuja!”

Richard akakata simu na kumwangalia mke wake. Alikuwa na hasira kali, hakuwaamini waganga na hakuona kama kwenye tatizo kubwa kama hilo mganga angeweza kumsaidia kwa lolote lile.
Akamwambia mke wake kuhusu simu ile iliyokuwa imepigwa, mkewe akamwambia kwamba aende huko kuonana na huyo mtu kwani siku zote binadamu hakutakiwa kukataa wito.

“Ila ni mganga!”
“Najua! Haimaanishi ukienda kumsikiliza tu basi atakuwa amekufanyia dawa. Nenda tu mume wangu,” alisema Bianca kwa sauti ya upole kabisa.
Kwa kuwa alisema mke wake, akachukua ufunguo wa gari na kuelekea huko. Hakuonekana kuwa na raha hata kidogo, moyo wake haukuwahi kumwamini mganga hata kidogo, alikwenda huko kwa ajili ya kumridhisha mke wake tu.

Alipofika, akateremka na kuelekea kaunta ambapo akamkuta Ibrahim ambapo baada ya kumuona Richard tu, akasimama kwa lengo la kuongea naye.
“Twende sehemu tukaongee!”
“Kwani hapa haiwezekani?”
“Ni muhimu sana! Twende tukaongee kaka,” alisema Ibrahim huku akimwangalia Richard.

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 122...

Kwa jinsi alivyoonekana, Richard hakumwamini Ibrahim, alionekana kama mwizi, alimuogopa na kuona kwamba kama angeingia naye ndani ya gari angeweza kufanya tukio lolote baya.
Kila alipomwambia kijana huyo kwamba wazungumze sehemu yeye alitaka ndani ya gari tu. Polisi aliyekuwa akiwasikiliza yeye mwenyewe alishangaa, hakujua sababu ya kijana huyo kutaka sana kuzungumza na Richard ndani ya gari.
“Kwa nini ndani ya gari?” aliuliza Richard.

“Wewe twende! Nitakwambia kwa nini!”
Hakuwa na jinsi, akamchukua Ibrahim na kuelekea naye ndani ya gari. Walipofika, wakaanza kuangalia kana kwamba kila mtu alikuwa akimsikiliza mwenzake azungumze kitu chochote kile.
“Kuna nini?”
“Nina mtoto wako,” alisema Ibrahim huku akimwangalia Richard ambaye moyo wake ukapiga paaa.
“Unasemaje?”

“Ninahitaji kuzungumza zaidi na wewe juu ya jambo hili. Kuna mengi ya kukwambia ila kwa kifupi ni kwamba ninaye mtoto wako,” alisema Ibrahim na kumfanya Richard kuanza kutokwa na kijasho chembamba, hakuamini kile alichokuwa akiambiwa, alihisi kama alikuwa akidanganywa ila kila alipomwangalia Ibrahim, aliendelea kumwambia kwamba alikuwa na mtoto wake.

**** Richard alihisi mwili wake ukitetemeka, alihisi kabisa kijasho chembamba kikimtoka. Hakuamini kile alichoambiwa na Ibrahim, alimwangalia kijana huyo, alimwambia kweli kwamba alikuwa na mtoto wake na alitakiwa kuondoka naye na kwenda kumuona.
Richard hakutaka kupoteza muda, hapohapo akawasha gari na kuondoka mahali hapo, ilikuwa ghafla sana kiasi kwamba mpaka polisi wenyewe walishangaa. Alitamani kumpigia simu mke wake na kumwambia kilichokuwa kimetokea lakini wakati mwingine alisita kwa kuona kwamba inawezekana kijana huyo alikuwa akimdanganya.

Hakukuwa na siku ambayo aliendesha gari kwa tahadhali kama siku hiyo, hakutaka kupata tatizo lolote, hiyo ilikuwa nafasi yake ya kumuona mtoto wake, pacha ambaye kila siku alimnyima furaha, pacha ambaye kila siku alimfanya kulia kwa maumivu makali.

Safari ikaishia Magomeni nje ya nyumba moja ya kawaida ambayo kwa kuonekana ilikuwa imejengwa kwa ajili ya kupangishwa tu. Haraka sana akazima gari na kuteremka, alionekana kuwa na haraka hata zaidi ya Ibrahim aliyekuwa amemuita.
 
Aliniambia aliniita notification za tag huwa sipati mm kabisa
Sio pekeako sipatagi pia kuna mtu kasema hapati itakua kwa wote.

Hata hivyo alichapia jina usingepata kama zingekua zinafika[emoji1]
 
SEHEMU YA 123...

Akatangulia ndani, hakujua aingie chumba gani, alijifanya kuwa na haraka kupita kawaida, mwenyeji alikuwa nje, tayari yeye alikuwa ndani, akajikuta amesimama tu ukumbini.
“Yupo wapi?” alimuuliza Ibrahim.
“Subiri kwanza! Hebu njoo ndani,” alisema Ibrahim na kumchukua mwanaume huyo kumpeleka chumbani kwake.

Richard alipoingia tu, akahisi hali ya tofauti, chumba kilikuwa na harufu nzito, kilikuwa shaghalabaghala, kwa jinsi kilivyoonekana ilikuwa ni rahisi kusema kwamba mtu aliyekuwa akiishi humo alikuwa masikini ambaye aliishi chini ya dola moja kwa siku.

Richard akahisi machozi yakianza kujaa machoni mwake na ndani ya sekunde chache yakaanza kutiririka. Moyo wake uliumia, hakuamini kama mtoto wake alikuwa akiishi ndani ya chumba hicho kilichoonekana kutokuwa na hadhi ya kukaliwa na mtu yeyote yule.

“Mtoto wangu yupo wapi?’ aliuliza Richard, mwanaume alikuwa akitiririkwa machozi tu.
Kwanza kabla ya kumwambia mahali alipokuwa mtoto wake, akaanza kumwambia kila kitu kilichokuwa kimetokea siku hiyo, tangu nesi mmoja alipompeleka mtoto wake nyuma ya ofisi ile kulipokuwa na pipa, alipomuona mwanaume akija kwa ajili ya kumchukua na yeye kumuwahi.

“Nashukuru sana! Mtoto wangu yupo wapi?” aliuliza Richard, hakutaka kusikia ilikuwaje mpaka mtoto wake alichukuliwa, alichokihitaji ni kujua mahali alipokuwa.
Ibrahim akatoka ndani ya chumba kile, akamfuata mama Issa ambaye akampa mtoto na kurudi naye chumbani. Richard alikuwa kwenye presha kubwa, mlango ulipofunguliwa, haraka sana akasimama na kuanza kumsogelea Ibrahim.

Alipomfikia, macho yake yakatua kwa mtoto wake, alikuwa amefanana na mtoto aliyekuwa nyumbani kwake, ilikuwa kazi nyepesi kugundua kwamba watoto hao walikuwa mapacha.

Machozi yake yakaongezeka, akamchukua mtoto huyo na kumkumbatia, moyo wake ukawa na furaha, furaha ambayo hakuwahi kuipata tangu siku alipozaliwa ndani ya dunia hii.

Alishindwa kuongea kitu chochote kile, kila alipotaka kuongea, alilia kwa kilio cha kwikwi, ilikuwa ni zaidi ya furaha, wakati mwingine kile kilichokuwa kikiendelea alihisi kwamba alikuwa katika njozi moja ya kusisimua ambapo baada ya dakika kadhaa angeamka na kujikuta akiwa kitandani.
 
SEHEMU ya 15...

Hilo ndilo alilolifanya Sarafina, hakutaka kuchelewa, akampigia simu David na kumwambia lengo lake la kutaka kutoa mimba hiyo hivyo alihitaji kiasi fulani cha pesa. David hakutaka kuchelewa, hapohapo, tena kwa haraka sana akamtumia kiasi cha shilingi laki mbili.
“Kaitoe haraka sana,” aliandika ujumbe mfupi.

“Sawa mpenzi!” aliitikia Sarafina na kumpanga Catherine kwamba siku inayofuata ilikuwa ni ya kwenda kwenye zahanati ya uchochoroni kwa ajili ya kutoa mimba.
**** Moyo wa Richard haukuwa na nafuu, ulitawaliwa na majonzi tele, alikosa furaha ambayo alitegemea kwamba angeipata. Alihuzunika mno kwa sababu alikataliwa na msichana aliyekuwa akimpenda kwa moyo wote.

Hakuacha kumfikiria, kila alipolala usiku, taswira ya msichana huyo ilimjia ndotoni. Wakati mwingine alitamani kumwambia kwamba alikuwa mtoto wa bilionea mkubwa lakini aliogopa kufanya hivyo.
Kila siku ilikuwa ni ya mateso tele, alipokwenda chuo na kumuona Sarafina akiwa na wakina David, moyo wake ulimuuma kupita kawaida. Alitamani kuwafuata wanaume hao na kuwaambia wamuachie msichana aliyekuwa akimpenda kwa moyo wa dhati lakini hilo halikuwezekana kabisa.

Siku ziliendelea kukatika, baada ya miezi kadhaa, akamuona Sarafina akianza kubadilika. Hakuonekana kuwa na furaha kama kipindi cha nyuma, hakuonekana kuwa na ukaribu na David kama ilivyokuwa.

Hilo halikumsumbua, aligundua kwamba mwanaume huyo alimchezea msichana huyo na hivyo kuamua kuachana naye. Hiyo ilionekana kuwa nafasi yake na kumfuata lakini alihofia. Kama Sarafina alimkataa kipindi cha nyuma, alikuwa amebadilika nini? Ilikuwa ni lazima kumkataa kwa mara nyingine tena.
Akaachana naye, akaendelea na mambo yake lakini kila alipomuona, moyo wake haukuacha kuuma kwani alitamani kumuona akiwa na furaha siku zote, furaha isiyomuhusisha mwanaume yeyote yule zaidi yake.

Baada ya kupita miezi mitatu, akashtuka kumuona msichana huyo akiwa amenenepa na kugundua kwamba alikuwa na mimba. Huo ndiyo ulikuwa msumari mkubwa kuliko yote moyoni mwake. Aliumia kwani kwa jinsi alivyompenda Sarafina hakutegemea kumuona akiwa na mimba ya mwanaume mwingine.

Je, nini kitaendelea?
Si alipewa laki 2 akatoe hiyo mimba na david sa tena kanenepa vp au ile hela aliitafuna sarafina mbona mpangilio wa hadithi yetu haueleweki wakati mwingine
 
Sio pekeako sipatagi pia kuna mtu kasema hapati itakua kwa wote.

Hata hivyo alichapia jina usingepata kama zingekua zinafika[emoji1]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] eti alichapia jina mana alianza kunifokea kanikuta chit chat nimekuita sehemu huoni au ujeuri
 
Si alipewa laki 2 akatoe hiyo mimba na david sa tena kanenepa vp au ile hela aliitafuna sarafina mbona mpangilio wa hadithi yetu haueleweki wakati mwingine
Usiwe unakurupuka kwanzaaa unatakiwa utulie usome mpaka episode zinazofatia
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] eti alichapia jina mana alianza kunifokea kanikuta chit chat nimekuita sehemu huoni au ujeuri
Na nikamwambia kabsaa hujatoa sauti wala hatasikia nazani hakuona ha ha haaa
Pole kwa kufokewa.

Cc Sakayo
 
Pamoja sana Shunie najua wewe huwa unamaliza mzigo wote bila hiyana,am on it once again
 
SEHEMU YA 124...

Hakubaki ndani ya chumba hicho, akajikuta akitoka na kuanza kuondoka chumbani humo, alipofika nje, akaingia ndani ya gari lake na kuondoka pasipo kuzungumza lolote na Ibrahim ambaye alibaki akishangaa, ilikuwaje mtu amsaidie kwa kiasi hicho halafu aondoke pasipo hata kumshukuru.

“Tenda wema nenda zako,” alisema Richard, akakaa kitandani, kitu alichokikumbuka kichwani mwake ni msichana Malaika tu.
Hakutaka kuendelea kubaki chumbani humo, haraka sana akasimama na kuondoka, alikuwa na haraka, mpenzi wake ndiye alikuwa kila kitu maishani mwake. Hakuchukua muda mrefu akafika katika hospitali hiyo ambapo akaelekea katika wodi aliyolazwa mpenzi wake.

Hali haikubadilika, madaktari walikata tamaa, kila siku walipokuwa wakimwangalia msichana huyo walijua kabisa kwamba alikuwa akienda kufariki dunia kitandani hapo.

“Dokta! Nini kinaendelea?” aliuliza Ibrahim.
Siku hiyo daktari alibadilika, alionekana kuwa tofauti kabisa na kila alipomwangalia Malaika aliona kifo kikiwa mbele yake.

Yeye na madaktari wengine walifanya kazi yao, walimpima Malaika na kugundua kwamba ule ugonjwa wa sickle cell aliokuwa akiumwa, ghafla ulibadilika na kuwa ‘terminal cancer’ ikiwa na maana kwamba ilikuwa ni kansa ambayo ni lazima imuue kitandani.

“Naomba nikwambie kitu kimoja,” alisema daktari huku akimwangalia Ibrahim.
“Kitu gani?” aliuliza Ibrahim.
Daktari huyo alimwambia kwamba mbali na ugonjwa wa sickle cell aliokuwa akiumwa mpenzi wake pia waligundua kwamba damu yake ilianza kushambuliwa na kansa na ndiyo sababu iliyomfanya kuteseka zaidi kitandani.

Hawakujua kansa hiyo ilianzaje, ilikuwa ghafla sana na mbaya zaidi ilivyokuwa imeanza kukomaa, haikuanza kikawaida, ilianza huku ikiwa na nguvu kubwa ya kuyapoteza maisha yake.

“Ni habari mbaya. Mwenzio amepata ugonjwa wa kansa ya damu, mbaya zaidi imekuwa terminal cancer,” alisema daktari huyo.

“Hiyo terminal ndiyo kitu gani hicho?”
“Ni kansa ambayo ni lazima afe, hawezi kupona kamwe. Mpenzi wako amebakiza miezi mitatu tu ya kuishi, baada ya hapo, atakufa, hatoweza kuishi tena,” alisema daktari huku akimwangalia Ibrahim.
“Unasemaje?”

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 125...

“Mwenzio atakufa ndani ya miezi mitatu tu. Kansa hii imeharibu mfumo mzima wa damu mwilini mwake,” alisema daktari huyo.
“Yaani unamaanisha kwamba mbali na sickle cell pia ameanza kuumwa kansa?” aliuliza Ibrahim.

“Ndiyo! Tulishindwa kufahamu kabla juu ya kansa hiyo, ilijificha na ninahisi ni tatizo ambalo linawatokea watu wengi tu. Ila ukweli ni kwamba mwenzio ana terminal cancer, ni mbaya sana, huwa ikija inakuja na muda wa kuishi, wengine hupewa miaka miwili, wengine mitatu, wengine mwaka na wengine hata mwezi. Kwa hii aliyokuwa nayo mwenzio imebakiza miezi mitatu tu ya kuishi,” alisema daktari huyo.

“Miezi mitatu?”
“Ndiyo!”
“Dokta! Hebu niambie ukweli kwanza, sijasikia! Umesema Malaika amebakiza miezi mitatu?” aliuliza Ibrahim.
“Ndiyo!”
“Ya kuishi?”
“Ndiyo!”
Akasikia kitu kikali kikiuchoma moyo wake, hakuamini kile alichokisikia, akajikuta akisimama na kuanza kuelekea kule alipokuwa Malaika, alikuwa akitembea huku akipepesuka, alihisi kabisa mwili wake ukianza kuishiwa nguvu, alipofika huko, akasimama pembeni ya kitanda chake, moyo wake ulikuwa na maumivu makali, alimwangalia mpenzi wake pale kitandani alipokuwa, hakuamini kama alikuwa njiani kumpoteza mpenzi wake huyo ambaye kwake alikuwa kila kitu.

“Terminal cancer…hawezi kuishi zaidi ya miezi mitatu lazima atakufa,” aliisikia sauti ya daktari moyoni mwake.
Malaika alikuwa kimya, aliyafumba macho yake lakini baada ya kuhisi kwamba kulikuwa na mtu amesimama mbele yake, akayafumbua macho na kumwangalia mtu huyo, akatoa tabasamu pana kwani mtu aliyekuwa amesimama alikuwa Ibrahim, mwanaume aliyekuwa muhimu sana katika maisha yake.

“Ibrahim! Mungu atatenda maajabu!” alisema Malaika huku akimwangalia Ibrahim ambaye alikuwa kimya tu.
“Najua unahuzunika! Nimeambiwa kwamba nimepatwa na kansa na nitakufa ndani ya miezi mitatu. Ibrahim, huu ndiyo muujiza ambao nimekuwa nikikwambia, hii kansa ndiyo muujiza ambao Mungu aliniotesha kwamba nitakutana nao,” alisema malaika huku akimwangalia Ibrahim.

“Unaumwa kansa Malaika! Si sickle cell tena! Kwa nini Mungu anafanya yote haya?” aliuliza Ibrahim.
“Kwa sababu anataka kuniponya!”
“Kukuponya! Kukuponyaje?” aliuliza Ibrahim.

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 126...

“Sijajua lakini nahisi hii ndiyo nafasi ya Mungu kujionyesha kwamba Yeye ni Mungu asiyeshindwa,” alisema Malaika kitandani pale ambapo alikuwa amekonda kupita kawaida.
Maneno yake yalikuwa hayohayo, alikuwa akijitia imani kila siku kwamba Mungu angekwenda kumponya.

Aliendelea kubaki hospitalini hapo na baada ya wiki moja madaktari wakamwambia Ibrahim kwamba kiasi cha fedha alichokuwa akidaiwa kilikuwa kikubwa, asingeweza kulipia lakini wakamtaka kumchukua Malaika na kurudi naye nyumbani ili akamtibu hukohuko nyumbani.

Hakuwa na jinsi, akamchukua Malaika wake na kurudi naye nyumbani kwake ambapo akaanza kumpa matibabu hukohuko, akaanza kumnunulia dawa na kumuhudumia kwa kila kitu kama alivyokuwa akiambiwa.

Mwili wa Malaika ukazidi kukongoroka, akabaki mifupa mitupu, kansa ya damu ikaanza kumtesa, mwili ukapauka na wakati mwingine akaanza kutoka damu puani na masikioni, ngozi yake ikashindwa kupambana na ugonjwa huo, ikaanza kusinyaa, ikaanza kutoa vipele vilivyokuwa vikimuwasha usiku na mchana, alipoanza kuvikuna, vikatumbuka na kuanza kutengeneza vidonda mwilini mwake, vidonda vilivyokuwa vikimuuma na kumfanya kupiga kelele usiku.

“Ibrahim mpenzi! Ninakufa…” alisema Malaika huku akilia kitandani pale.
“Malaika! Kumbuka uliniambiaje! Kumbuka maneno uliyosema kwamba Mungu atakuponya. Mpenzi utapona, utapona, hautokufa! Nakwambia hautokufa,” alisema Ibrahim huku akimwangalia mpenzi wake huyo pale kitandani.

Kila siku ikawa mateso juu ya mateso, vidonda vile vilivyosababishwa na vipele viliendelea kumuuma zaidi, akawa mtu wa kulia, vikatoa damu na mwisho wa siku hali kubadilika na kutoa usaha kitu kilichosababisha harufu kali ndani ya chumba hicho.

“Mmh! Kuna panya ameoza au kuna maiti humu ndani?’ alisikika akiuliza mwanamke mmoja ndani ya nyumba hiyo.
Mwili wa Malaika ukazidi kutoa harufu kali ambayo iliwafanya wapangaji wengi kuanza kulalamika ndani ya nyumba hiyo kwamba iweje wakae na maiti ndani iliyokuwa imeoza na kunuka, wengi wakamtaka Ibrahim kwenda kumzika Malaika kwani tayari alikuwa amekufa na ndiyo maana mwili wake ulikuwa ukitoa harufu mbaya kama kitu kilichooza.

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 127...

Kwa Ibrahim, ni kama pua zake ziliziba, chumba kizima kilikuwa na harufu mbaya lakini hakusikia hata kidogo. Kila siku alikaa chumbani humo, mpenzi wake alionekana kukata tamaa, mwili wake ulizidi kuisha na vidonda vilimtesa kupita kawaida.

Hakuondoka chumbani, hakumkimbia, kila siku alipambana naye pamoja, alimtia nguvu na kumwambia kwamba kuna siku angepokea uponyaji na Mungu aliyaandaa maisha mazuri kwa ajili yake.

Malaika alilia na kulia, hakuwa na nguvu, kila alipomwangalia Ibrahim, aliyaona kabisa mapenzi ya mwanaume huyo, jinsi alivyompenda kiasi kwamba hakuwa tayari kumkimbia kwa kuwa tu alikuwa akitoa harufu mbaya.

Imani yake iliyoanza kuyumba kipindi cha nyuma ikaanza kurudi tena, alimwamini Mungu kwamba kuna siku angeweza kusimama tena, kutembea na kufanya mambo mengine kama kipindi cha nyuma.

Hakujua sababu ya Mungu kumpitisha katika maisha hayo, yalikuwa ni maisha yaliyoumiza mno, maisha ambayo yalimfanya kila siku kuona muda wowote ule angekufa kama alivyokufa mama yake. Hakuona kama angepokea tumaini lolote lile, alijua kabisa kwamba hizo ndizo zilikuwa siku za mwisho za uhai wake.

“Ibrahim mpenzi!” aliita Malaika huku akimwangalia mwanaume huyo.
“Ndiyo mpenzi!”
“Unaamini pamoja na mimi kwamba nitapona?” aliuliza Malaika huku akimwangalia Ibrahim, kwa kukiangalia kitanda harakaharaka, tena katika kipindi ambacho Malaika alikuwa amejifunika shuka, ilikuwa vigumu kuamini kama kitandani hapo kulikuwa na mtu kwa jinsi alivyokonda na kubaki mifupa mitupu.

“Ninaamini kwamba Mungu atakuponya! Huwezi kufa Malaika,” alisema Ibrahim huku machozi yakimtoka, alikosa tumaini, hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kumsaidia msichana huyo maishani mwake.

“Hata mimi naamini nitapona. SITOKUFA BALI NITAISHI,” alisema Malaika kwa imani kubwa kutoka moyoni mwake, kama Mungu alikuwa akitenda miujiza kwa kuwa tu watu waliamini, aliamini kwamba hata yeye pia angeweza kumfanyia muujiza huo.

Kila siku wapangaji walikuwa watu wa kulalamika, walimlalamikia mwenye nyumba kwamba Malaika hakutakiwa kuishi ndani ya nyumba hiyo kwani kwa jinsi alivyokuwa akinuka, ilikuwa ni balaa tupu.

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 128...

Mwenye nyumba hakutaka kuwasikiliza, aliyajua maisha ya msichana huyo, jinsi alivyokuwa akiteseka lakini zaidi alijua maisha ya Ibrahim, alikuwa akimpenda Malaika kiasi kwamba hakutaka kusikia lolote lile kutoka kwa mtu yeyote.

Kila siku ndani ya nyumba kulikuwa na kelele kiasi kwamba baadhi ya wapangaji wakatishia kuhama nyumba hiyo kwani mateso yalizidi, harufu kali iliendelea kuzitesa pua zao kila siku.

Mwenye nyumba hakuwa radhi kuona akipoteza wapangaji kwa ajili ya mpangaji mmoja tu, hivyo alichokifanya ni kumfuata Ibrahim na kuzungumza naye.

Alimwambia hali halisi, jinsi wapangaji wenzake walivyokuwa wakilalamika kimyakimya kwamba mpenzi wake alizidi kutoa harufu kiasi kwamba hata kama utapika pilau, harufu ya pilau haisikiki zaidi ya harufu mbaya ya mwili wa Malaika.

“Mzee! Sina pesa yoyote ile, tutaishi wapi?’ aliuliza Ibrahim huku akimwangalia baba mwenye nyumba.
“Popote pale lakini si hapa. Ibrahim, si kwamba mimi ndiye nawafukuza, ninalazimishwa, ninafanya hivi huku nikiumia sana, hasa hali aliyokuwa nayo mwenzio, hakika inaniumiza sana,” alisema mzee huyo huku akimwangalia Malaika, kwa jinsi alivyokuwa kitandani pale, ilionekana kama angeishi mpaka siku inayofuata basi alitakiwa kumshukuru sana Mungu.

“Mzee! Nipo kwenye wakati mgumu sana. Unaweza kutupa hata mwezi mmoja?” aliuliza Ibrahim.
“Mwezi mmoja? Kwa jinsi hawa watu walivyokuwa na kelele, hata wakijua nimewapa siku mbili, maneno mengi,” alisema mzee huyo.

Aliumia lakini hakuwa na jinsi, alimwangalia mpenzi wake, Ibrahim akashindwa kuvumilia, akaanza kulia kwa sauti, aliumia moyoni mwake, hakuamini kama kweli alikuwa akipitia maisha hayo, mpenzi wake aliteseka, mpenzi wake alikuwa hoi, mpenzi wake alikaribia kufa, mpenzi wake huyo alikuwa na siku chache za kuishi dunia.

Siku iliyofuata, akaamua kuondoka nyumbani hapo, hakujua ni mahali gani alitakiwa kwenda, aliuchukua mkeka tu, mpenzi wake, Malaika hakuweza kutembea, alimbeba mgongoni, alipotoka ndani tu, watu wote waliokuwa nje wakaziba pua zao kwani harufu iliyokuwa ikisikika ilinuka mno.

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 129...

“Usiniache mpenzi! Naomba usiniache! Usife mpenzi! Ninakupenda naomba usife. Mungu naomba usimchukue Malaika wangu, chukua chochote kile lakini niachie Malaika wangu,” alisema Ibrahim huku akijaribu kuzuia kilichotaka kutokea.

Hapohapo, ghafla sana Malaika akatulia, joto la mwili likazidi kupanda, mwili ukanyooka na kutulia tuli.
“Malaikaaaaaaaaa…..” aliita Ibrahim kwa sauti kubwa huku akijaribu kumuamsha mpenzi wake lakini hakuamka, hata macho yake yalifumba.

*** Richard alikuwa njiani akielekea nyumbani kwake, hakuamini kilichokuwa kimetokea, mtoto wake mpendwa alikuwa mapajani mwake. Hakutaka kumpigia simu mke wake na kumwambia kilichokuwa kimetokea, alitaka kumsapraizi kwani aliamini kwamba kile kingekuwa kitu ambacho kingempa furaha maisha yake yote.

Aliendesha gari kwa umakini mkubwa na baada ya dakika kadhaa akafika nyumbani kwake ambapo mlinzi akafungua geti na kuteremka.

Akaanza kuelekea ndani, akamkuta mke wake akiwa sebuleni akimnyonyesha mtoto.
Akasimama, akamwangalia huku akitoa tabasamu. Bianca akashtuka, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, akamsogelea mume wake ambaye alimuonyeshea mtoto yule. Kitendo cha Bianca kutua macho yake kwa mtoto yule, moyo wake ukapiga paaa kwani alifanana na mtoto aliyekuwa akimnyonyesha.

“Is this my baby?” (huyu ni mtoto wangu?) aliuliza Bianca huku akiwa haamini.
“He is the one,” (ndiye yeye)
“Where did you get him?” (umempata wapi?) aliuliza Bianca huku akimchukua.
Hakuamini macho yake, machozi ya furaha yaliyochanganyikana na uchungu yakaanza kujikusanya machoni mwake na kuanza kulia.

Alijisikia hali ya tofauti kabisa, hakuamini kile kilichotokea, alijua kwamba asingeweza kumuona tena mtoto wake, alikata tamaa na kumwachia Mungu kumbe upande wa pili bado Mungu alikuwa akiendelea kufanya kazi yake.

Kila mmoja alikuwa na furaha tele, Bianca akashindwa kuvumilia, akawapigia simu marafiki zake na kuwaambia kwamba alimpata mtoto wake, ni kwamba Mungu alikuwa upande wake na alimpigiania.

Itaendelea.
 
SEHEMU YA 130...

Wote walifurahi, furaha ikarudi ndani ya nyuma. Richard hakukumbuka chochote kuhusu Ibrahim, kwake maisha yalikuwa yakiendelea kama kawaida. Siku moja baada ya kukaa ofisini na kuanza kuyakumbuka maisha yake ya nyuma ndipo akakumbuka namna alivyompata mtoto wake.

Moyo wake ukauma, hakuamini kama yeye ndiye aliyefanya ujinga ule, kuondoka chumbani kwa Ibrahim pasipo hata kumshukuru na wakati yeye ndiye aliyemsaidia kumpata mtoto huyo, ndiye alikuwa kijana aliyemuiba mtoto kule nesi alipomficha, kwa maana hiyo alikuwa na uwezo wa kumfanya chochote mtoto yule.

Moyo wake ukamuhukumu, hakuwa amefanya utu, alisikia maumivu mazito moyoni mwake, aliumia kupita kawaida na kujiona akiwa mkosaji mkubwa ndani ya dunia hii.

Hapohapo akachukua simu yake na kumpigia mke wake, alipopokea, akaanza kumwambia jinsi alivyompata mtoto, hakumficha, alimwambia ukweli kwamba alishindwa kumshukuru kijana yule, hivyo akaondoka zake huku akiwa na mtoto.
“Hukumshukuru?” aliuliza Bianca huku akishangaa.

“Mke wangu! Nilizidiwa na furaha, nilitaka kuzungumza, nikashindwa, kiukweli nilifanya kosa kubwa sana,” alisema Richard huku simu ikiwa sikioni mwake.

Bianca akamwambia kwamba ilikuwa ni lazima waelekee huko kwa ajili ya kumshukuru kijana huyo kwani kwa kile alichokuwa amekifanya kilikuwa ni kitu kikubwa ambacho hata kama wangempa milioni mia moja bado kusingelingana na kile alichokuwa amekifanya.

Richard hakutaka kubaki ofisini, akatoka, akachukua gari lake na kumpitia mke wake ambapo moja kwa moja wakaanza safari ya kuelekea huko. Njiani, walizungumza sana, Richard aliendelea kuhuzunika moyoni mwake, hakuamini kama aliweza kufanya jambo kama lile, alitakiwa kuonyesha shukrani, alitakiwa kumuonyeshea kijana yule dalili zote za kumshukuru kwa kile alichokuwa amekifanya.

Hawakuchukua muda mwingi wakafika Magomeni ambapo moja kwa moja wakapaki gari na kuelekea ndani ya nyumba ile.

Hakukuwa na mtu ila kwa kuwa Richard alikuwa akikifahamu chumba, akaelekea na kuugonga mlango ule ambapo baada ya sekunde chache, mlango ukafunguliwa na mwanamke mmoja mweupe aliyejichubua kufungua mlango.
“Kuna mtu namuulizia,” alisema Ricard mara baada ya salamu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom