SEHEMU YA 149...
“Malaika! Mungu aliyaandaa maisha haya tangu ulipokuwa katika tumbo la mama yako. Alikuwekea kitu kimoja, ili uweze kuyafikia ilitakiwa kuamini. Namkumbuka mchungaji aliposema kwamba kama kweli unataka kufanikiwa ni lazima Mungu akupitishe katika tanuru la moto, kwenye hilo tanuru la moto kuna wengine watakata tamaa, wengine watapambana, na watu watakaovuka basi ndiyo watakutana na mafanikio ambayo Mungu aliwaahidi tangu wakiwa tumboni kwa mama zao,” alisema Richard huku akimwangalia Malaika.
“Nilizaliwa kuamini, nimekuwa nikiamini kwa kipindi chote cha maisha yangu. Nilijua kwamba kuna siku haya yaliyotokea yangetokea na hakika Mungu amefanya,” alisema Malaika na kumkumbatia Ibrahim ambapo ilipofika Jumamosi ya tarehe 03/07/2017 wawili hao wakafunga ndoa katika Kanisa la Living God lililokuwa jijini Dar es Salaam.
MWISHO