Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
- Thread starter
- #81
SEHEMU YA 65...
Mzee Mpobela akampanga David na kumwambia jinsi biashara hiyo ilivyokuwa ikifanywa na hata jinsi usafirishaji ulivyokuwa mwepesi. Kutoa mzigo mkubwa kutoka Tanzania kupeleka nchi kama Brazil hakukuwa na ugumu wowote ule.
Kitu ambacho kilitakiwa kufanywa ni kufanya mawasiliano uwanja wa ndege wa Tanzania na Brazil kwa kutoa kiasi kikubwa cha pesa na kazi kufanyika kwa haraka sana na wepesi mno.
Kwa wafanyakazi ambao walikuwa na tamaa ndiyo waliokuwa wakiingizwa kwenye mkenge na kufanya kazi hiyo kwa ajili ya kuingiza kiasi fulani cha pesa. Akapewa michongo yote na kisha kupewa mzigo wenye gharama ya shilingi bilioni mbili na kuupeleka nchini Brazil kwa mfanyabiashara Marcos Bebe.
Kwa Tanzania hakukuwa na tatizo, tayari wafanyakazi hao wenye tamaa walipewa taarifa na hivyo kazi kuachwa kwa Bebe ambaye naye akafanya kwa sehemu yake kwa kuhonga wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rio De Janeiro uliokuwa katika jiji hilo hilo.
Alipofika, akachukua mabegi yake, akateremka na kuanza kuelekea nje ya uwanja huo. Hakukuwa na mtu yeyote aliyembughudhi, kitu cha kushangaza kabisa ni kwamba hakupekuliwa, akapitishwa katika mlango mwingine na kuelekea nje kabisa.
Huko, akakutana na vijana watatu wakiwa nje ya gari moja la kifahari. Akakaribishwa na kuingia ndani ya gari hilo. Alipokuwa ndani ya ndege alikuwa na hofu ya kukamatwa lakini baada ya kuingia ndani ya gari hilo akajiona akiwa salama kabisa.
Hakuzungumza kitu garini, macho yake yalikuwa yakiangalia huku na kule kulitalii jiji hilo kubwa la Rio. Safari iliendelea huku wanaume wale wakipiga stori kwa Lugha ya Kireno, hakuelewa walizungumza nini, alikaa kimya tu.
Baada ya dakika kadhaa gari hilo likaanza kuingia katika jumba moja kubwa na la kifahari. David alibaki akishangaa, katika maisha yake aliwahi kuyaona majumba makubwa ya kifahari lakini halikuwa kama hilo.
Itaendelea.